DIWANI WA KATA SAMBASHA ( CCM) AACHIWA KWA DHAMANA DHIDI YA KESI INAYOMKABILI - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

DIWANI WA KATA SAMBASHA ( CCM) AACHIWA KWA DHAMANA DHIDI YA KESI INAYOMKABILI

Aliyewahi kuwa mwenyekiti wa UVCCM,na Diwani wa Kata ya Sambasha  mkoa wa Arusha Lengai Ole Sabaya (aliyevaa suti nyeusi)akiwa nje ya mahakama mara baada ya kuachiwa kwa dhamana kutokana na kesi inayomkabili.(Picha na Vero Ignatus Blog).

 NA VERO IGNATUS, ARUSHA
Mahakama ya Hakimu mkazi Arusha leo Agosti 11, 2017 imemsomea mashtaka mawili aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa umoja wa vijana (UVCCM) Lengai Ole Sabaya ambaye pia ni diwani wa kata ya Sambasha Wilaya ya Arusha vijijini .


Miongoni mwa makosa hayo aliyosomewa mahakamani hapo ni pamoja na kosa la tuhumiwa ya kujifanya Afisa Usalama wa Taifa, (TISS), huku kosa lingine ikiwa ni kugushi moja ya nyaraka za serikali(kitambulisho ).


Akisoma mashtaka hayo mahakamani hapo,wakili wa serekali Penina Joakim  amesema kuwa Mnamo Mei 18 katika hotel ya Skyway iliyopo makao mapya jijini Arusha Mshitakiwa alijitambulisha kama Afisa utumishi wa idara ya usalama wa taifa na kufanya Utapeli . Wakili Penina alitaja kosa la pili ambalo Mshitakiwa Lengai Ole Sabaya alisomewa kuwa ni kugushi kitambulisho cha idara ya usalama wa Taifa kilichokuwa kikisomeka Jamhuri ya Muungano wa Tanzania idara ya usalama wa Taifa (TISS) Lengai Ole Sabaya kikosi maalumu Agent (undercover), chenye code no MT 86117 huku akitambua kuwa ni kinyume cha kisheria . Hata hivyo mara baada ya kusomewa mashtaka hayo mahakamani hapo mtuhumiwa alikana mashtaka na ndipo Hakimu Mkazi aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo Nestory Barro alisema dhamana ipo wazi iwapo wadhamini watakidhi vigezo vinavyotakiwa na mahakama hiyo.

Aliyewahi kuwa mwenyekiti wa UVCCM,na Diwani wa Kata ya Sambasha  mkoa wa Arusha Lengai Ole Sabaya (aliyevaa suti nyeusi)akizungumza na vyombo vya habari nje ya mahakama.Picha na Vero Ignatus Blog.

Akizungumza na mwenyekiti wa CCM katika kata ya Sambasha Lesion Letionoki Njoki.


Akisalimiana na wananchi wa kata ya Sambasha mara baada ya kuachiwa kwa dhamana.Picha na Vero Ignatus Blog.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages