CHUO CHA UFUNDI ARUSHA CHAZINDUA MTAALA MPYA WA GESI NA MAFUTA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

CHUO CHA UFUNDI ARUSHA CHAZINDUA MTAALA MPYA WA GESI NA MAFUTA

Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Arusha,Hagnery Chitukulo akizungumza wakati wa ufunguzi wa kozi ya ufundi bomba,mafuta na gesi katika chuo
cha Ufundi Arusha(ATC) jijini Arusha,kushoto ni Mkuu wa Chuo cha 
Camosun nchini Canada,Sherri Bell na kulia ni Mkuu wa Chuo cha ATC,Dk Richard Masika

Afisa wa kitengo cha biashara katika ubalozi wa Canada nchini,Anita
Kundy akisoma hotuba yake,kushoto ni  Mshauri wa ufundi kutoka nchini Canada,Dk Alan Copeland.
Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Arusha,Hagnery Chitukulo akionesha nakala ya mtaala mpya wa  kozi ya ufundi bomba,mafuta na gesi uliozinduliwa  katika chuo cha Ufundi Arusha(ATC)

Mkurugenzi wa Elimu ya Ufundi nchini(TVET)Wizara ya Elimu,Sayansi na
Teknolojia,Mhandisi Thomas Katebalirwe akizungumza jambo katika hafla ya uzinduzi huo.

Baadhi ya wanafunzi wa mwanzo wa kozi ya ufundi bomba na utaalamu wa gesi na mafuta katika Chuo cha ufundi Arusha

Mgeni rasmi Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Arusha,Hagnery Chitukulo(wa tatu  kushoto)akiwa katika picha ya pamoja na wageni kutoka Chuo cha  Camosun,Victoria nchini Canada na Chuo cha ATC.
Kaimu Katibu Tawala mkoa wa  Arusha,Hagnery Chitukulo amekipongeza Chuo cha Ufundi Arusha(ATC) kwa uamuzi wake wa kushirikiana na Chuo cha Camosun cha nchini Canada  kuandaa mtaala wa ufundi bomba,gesi na mafuta katika ngazi ya Diploma.


Akizindua mtaala huo ambao ni kwanza na  aina yake nchini alisema utaisadia serikali kuwapata vijana wengi wenye  utaalamu wa sekta ya mafuta na gesi nchini katika ngazi hiyo ambayo  imenekana kuna pengo kubwa nchini.



"Mafunzo haya yatasaidia sana kuwapata  wataalamu wetu na itaipunguzia serikali mzigo wa kuwaajili wataalamu wa  kigeni ambao ulipwa fedha nyingi za kigeni,"alisema



Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha,Dk  Richard Masika amesema baada ya kutambua mahitaji makubwa ya wataalamu  wa fani hiyo katika kipindi cha miaka miwili iliyopita walikua wakiaanda mtaala kwa ushirikiano na Chuo cha Camosun na mafanikio yamepatikana.


Alisema kozi hiyo ni nyumbufu  itakayowawezesha wanafunzi kufanya kazi baada ya kumaliza mwaka wa  kwanza na baadaye kuendelea na masomo jambo ambalo litakua likiwapa  maarifa kwa vitendo zaidi badala ya nadharia pekee.


Mmoja wa wanafunzi wanaosoma kozi hiyo  ambayo imegharamiwa na serikali ya Tanzania,Latifa Mkombo amesema  wanaishukuru serikali kwa kutoa ufadhili huo na kuahidi kusoma kwa bidii kwaajili kuingia katika ajira za gesi na mafuta.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages