Mkuu wa Wilaya ya Geita Herman Kapufi akizungumza wakati akifungua mafunzo ya siku moja kwa maofisa ugani wa wilayani yake wilayani humo jana yaliyoandaliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), yenye lengo la kuwakumbusha wataalamu hao wa kilimo nafasi yao pamoja na kuwapatia mbinu mpya za kisasa katika kulima mazao ya Mihogo, Pamba na Viazi vitamu katika kuelekea serikali ya viwanda.
Picha ya pamoja.
Maofisa ugani wakiwa kwenye mafunzo hayo.
Mratibu wa Jukwaa la bioteknolojia kwa maendeleo ya kilimo nchini OFAB bwana Philbert Nyinondiakizungumza kwenye ufunguzi wa mafunzo hayo.
Mshauri wa Jukwaa la Masuala ya Bioteknojia OFAB, Dk.Nicholaus Nyange (kushoto), akitoa mada kuhusu matumizi ya Bioteknolojia katika kilimo. |
Na Dotto Mwaibale, Geita
HALMASHAURI ya Wilaya ya Geita Mkoani Geita imesema itahakikisha inatenga bajeti ya shilingi milioni 50 kuwezesha mafunzo na kuboresha sekta ya kilimo kutoka kwenye fedha zake pamoja nakuwaomba wadau wengine wa wilaya kama vileKampuni ya uchimbaji dhahabu ya geita GGM kuchangia milioni 200 ili kuinua sekta hiyo.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa wilaya hiyo, Herman Clement Kapufi wilayani humo jana wakati akifungua mafunzo ya siku moja kwa maofisa ugani wote wa wilayani yake yaliyoandaliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), yenye lengo la kuwakumbusha wataalamu hao wa kilimo nafasi yao pamoja na kuwapatia mbinu mpya za kisasa katika kulima mazao ya Mihogo, Pamba na Viazi vitamu katika kuelekea serikali ya viwanda.
Mkuu huyo wa wilaya amesema kazi hiyo nzuri iliyoanzishwa na COSTECH kupitia Jukwaa la Bioteknolojia nchini (OFAB) hazitakuwa na maana endapo mafunzo hayo hayatasimamiwana halmashauri yake ili kuhakikisha yanakwenda kuleta mabadiliko na mapinduzi kwenye kilimo kwa wakulima kwenye maeneo mbalimbali.
Kapufi amemtaka mkurugenzi wa halmashauri kuhakikisha anaweka bajeti kugharamia mafunzo ya aina hiyo kwa maofisa ugani na wakulima badala ya kuwaachia COSTECH
kufanya kazi hiyo peke yao wakati wanufaika ni wananchi wa wilaya hiyo na hivyo kuahidi kuzungumza na wawekezaji wenye migodi kuweka bajeti kusaidia kilimo kwenye fedha mbalimbali zinazotolewa nao kwaajili ya maendeleo ya halmahauri.
Amesema anatambua kuna wakulima wengine hawapendi kubadilika pale wanapofikishiwa utaalamu lakini amewataka maofisa ugani hao kuto kata tamaa na badala yake wawe na
mashamba yao binafsi ya mfano ambayo yatalimwa kwa kutumia kilimo cha kisasa na mbegu bora ili waone badala ya kuzungumza kwa nadharia kila siku.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya hiyo Ali Rajabu, amewapongeza watafiti hao kutoka COSTECH,OFAB na Kituo cha utafiti wa Kilimo Ukiriguru cha Mwanza kwa kusaidia kuwawezesha maofisa ugani hao kupata mbinu bora zaidia za kukabiliana na changamoto za kilimo kwa wakulima kwa kutumia teknolojia za kisasa na kuiomba Halmashauri kuwapa vitendea kazi maofisa ugani wanaofanya vizuri kwenye kata zao.
Amesema maofisa ugani ndio injini ya kilimo maana ndio wenye jukumu la kuwasaidia wakulima kulima kisasa na kuzalisha kwa tija ikizingatiwa kuwa bila chakula hakuna mtu anayeweza kufanya kazi na njaa hivyo tunahitaji chakula ili kuweza kufikiria
kufanya kazi zingine za kimaendeleo.
Ameiomba COSTECH kutoishia kwenye wilaya hii pekee bali mafunzo ya aina hiyo yafanywe nchi nzima kwani uhitaji ni mkubwa kwenye kila wilaya ili kuwakumbusha kazi wataalamu hao wa kilimo na pia kuwapa mbinu mpya za kutatua changamoto zinazowakabili wakulima kwenye mazao hayo ya pamba mahindi, mihogo na viazi lishe
Amesema imefika wakati sasa wananchi wa mkoa huo kubadilika na kutofikiria dhahabu kila wakati badala yake wajishughulishe na shughuli za kilimo tena cha kisasa kwa kutumia fursa ya ziwa Victoria katika kulima kilimo cha umwagiliaji na hivyo kuongeza tija
Awali akizungumza kabla ya kumkaribisha Mkuu wa wilaya Mratibu wa Jukwaa la Biotehnolojia kwa maendeleo ya kilimo nchini (OFAB)Philbert Nyinondi kwa niaba ya COSTECH amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwasaida wataalamu hao wa kilimo kupata mbinu mpya za uzalishaji na kuwajengea uwezo kwenye kuzalisha mazao hayo muhimu ambayo yana mchango mkubwa katika kusaidia kupata malighafi kwaajili ya viwanda.
Amesema mafunzo hayo baada ya kutolewa kwa maofisa ugani pia yatatolewa kwa wakulima kwenye vikundi na kisha kuwapatia mbegu bora na safi za mihogo na viazi lishe ili kuanzisha mashamba darasa kwenye vijiji vitakavyochaguliwa ili wakulima
waweze kuona na kujifunza na kisha kuwa sehemu ya mbegu bora kwenye wilaya.
Nyinondi amesema mpango huu ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu ya Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia katika kuhakikisha sayansi,teknolojia na tefiti nzuri zinawafikia walengwa na kuleta tija kwenye sekta husika ili kuongea tija.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)