PPF Ndani ya Sabasaba yaendelea kuwavuta wengi - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

PPF Ndani ya Sabasaba yaendelea kuwavuta wengi

 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bw. William Erio, (mwenye suti), akiungana na wafanyakazi wenzake kuhudumia wananchi wakati wa maonesho ya 41 ya biashara ya kimataifa uya Dar es Salaam leo Julai 2, 2017. Wananchi wengi waliotembelea banda hilo wamefurahishwa na huduma zitolewazo na wafanyakazi wake kwa kwa jinsi wanavyosikiliza na kutoa huduma kwa wanachama na wananchi wengine. miongoni mwa maswali mengi yaliyoulizwa mara kwa mara ni kuhusu mpango wa uchangiaji wa hiari ujulikanao kama "Wote Scheme), unaotoa fursa kwa wajasiriamali wadogo kama mama lishe madereva wa bodaboda, wamachinga na mtu yeyote anayefanya kazi halali ya kumuingizia kipato anavyoweza kujiunga na mpango huo na hatimaye kupata faida mbalimbali ikiwemo bima ya afya na mikopo kwa wajasiriamali wadogo,
 Wananchi wakipatiwa maelezo kuhusu shughuli na huduma zitolewazo na PPF.
 Meneja wa elimu kwa wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bw. Kwame Temu, (kushoto), akitoa maelezo kwa mwananchi huyu aliyetembelea banda la Mfuko huo lililoko jengo la Wizara ya Fedha na Mipango kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere kuinakofanyika maonesho ya 41 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam leo Julai 2, 2017
  Wananchi wakipatiwa maelezo kuhusu shughuli na huduma zitolewazo na PPF.
  Wananchi wakipatiwa maelezo kuhusu shughuli na huduma zitolewazo na PPF.
 Wafanyakazi wa PPF, wakiwa makini katika kuwahudumia wananchi waliofika banda la Mfuko huo






 Mkurugenzi Mkuu wa PPF, Bw. William Erio, (kushoto), akizungumza jambo, wakati alipokutana na muigizaji mkongwe hapa nchini, Mzee Jangala, (wapili kushoto), wakati akitembelea bustani daraza ya Jeshi la Magereza, kwenye maonesho ya 41 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam, leo Julai 2, 2017. Wengine pichani kutoka kulia ni Bi. Yunge Saganda wa Jeshi la Magereza, Bi. Lulu Mengele, Meneja Uhusiano wa PPF na Bi Jannet Ezekiel Afisa Uhusiani Mwandamizi wa Mfuko huo
Mama Anna Mkapa, (kushoto),  ambaye ni  Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote, (EOTF), na Mke wa Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa, akizungumza jambo na Mkurugenzi Mkuu wa PPF, Bw. William Erio, (wapili kushoto), Mama Mwantumu Mahiza, wakati alipotembelea banda la EOTF linalowakusanya wajasiriamali mbalimbali kuitoka nchini kote leo Julai 2, 2017
 Mjasiriamali kutoka mkoani Kigoma, Bi.Dporothy Timoth Takwe, (kushoto), akitoa maelezo ya ladha nzuri ya dagaa wa ziwa Tanganyika, wakati mama Mkapa, Mkurugenzi Mkuu wa PPF na mmoja wa viongozi wa televisehni ya Agape, (kulia), wakati walipotembelea banda la mjasiriamali huyo lililoko jengo la EOTF
 Mama Mkapa, Mkurugenzi Mkuu Erio, wakitazama bidhaa zilizofungwa vizuri na wajasiriamali wa Tanzania
Bw. Erio akisaini kitabu cha wageni kwenye banda la Magereza

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages