GREEN WASTEPRO LTD WASHIRIKI WIKI YA MAZINGIRA KWA KUSAFISHA FUKWE YA AGA KHAN - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

demo-image

GREEN WASTEPRO LTD WASHIRIKI WIKI YA MAZINGIRA KWA KUSAFISHA FUKWE YA AGA KHAN

DSC_0229
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema akisitiza jambo kwa wadau walioshiriki zoezi la usafi katika fukwe ya bahari ya Hindi eneo la Aga Khan na kuwaomba waendelee na kufanya usafi na hata kuwahamasisha watu wengine kuwa mabalozi wa mazingira ili kufikia malengo waliyojiwekea katika manispaa ya Ilala.
DSC_0233
DSC_0213

Baadhi ya wadau wa mazingira waliofika kwenye zoezi la usafi katika wiki ya Mazingira lililoendeshwa na kampuni ya Green Waste Pro Ltd wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema.
DSC_0280
Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala , Mstahiki Omary Kumbilamoto akizungumza jambo kwa wadau mbalimbali waliokuja kujumuika katika zoezi la usafi katika fukwe ya Bahari ya Hindi eneo la Agha Khan katika wiki ya mazingira.
DSC_00011
Meneja wa uendeshaji wa kampuni ya Green Waste ProLtd, Abdallah Mbena akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ushiriki wa kampuni hiyo katika zoezi la kufanya usafi katika fukwe ya Bahari ya Hindi kata ya Kivukoni eneo la Aga Khan jijini Dar ikiwa ni wiki ya Mazingira.
DSC_0080
Wafanyakazi wa Manispaa ya Ilala pamoja na wafanyakazi wa Green Waste Pro Ltd wakiendelea kufanya usafi katika fukwe ya Bahari ya Hindi kata ya Kivukoni eneo la Aga Khan jijini Dar ikiwa ni wiki ya Mazingira. Mwenye shati nyeupe ni  Meneja Msaidizi wa kampuni Green WastePro ltd, Erick Mark.DSC_0091
DSC_0051

DSC_0006
Baadhi ya wadau wa mazungira wakifanya zoezi la usafi katika fukwe ya Bahari ya Hindi eneo la Aga Khan kata ya Kivukoni ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya Mazingira huku akishirikiana na viongozi wa kampuni iliyopewa zabuni ya kusafisha manispaa ya Ilala Green Waste Pro Ltd pamoja na wafanyakazi wa manispaa ya Ilala.
DSC_0019

DSC_0059
DSC_0111
Baadhi ya uchafu ukiwa kwenye mifuko yake mara baada ya kumalizika kwa zoezi la usafi katika fukwe ya Bahari ya Hindi eneo la Aga Khan kata ya Kivukoni ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya Mazingira huku akishirikiana na viongozi wa kampuni iliyopewa zabuni ya kusafisha manispaa ya Ilala Green Waste Pro Ltd pamoja na wafanyakazi wa manispaa ya Ilala.
DSC_0157

DSC_0353
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Green WastePro Ltd  mara baada ya kumaliza kufanya usafi kwenye fukwe ya Bahari ya Hindi eneo la Aga Khan kata ya Kivukoni ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya Mazingira.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Pages