Airtel yaleta TABASAMU, yazindua vocha ya shilingi 200 nchini - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Airtel yaleta TABASAMU, yazindua vocha ya shilingi 200 nchini

 Meneja Masoko ya Airtel, Anethy Muga (kulia) na Meneja wa chapa wa Airtel, Arnold Madale (kushoto) wakionyesha vocha mpya ya Airtel Tabasamu itakayouzwa kwa bei ya shilingi mia mbili tu. Katikati  ni Meneja  Uhusiano wa Airtel , Jackson Mmbando
 Meneja  Uhusiano wa Airtel , Jackson Mmbando (kati) akitoa ufafanuzi juu ya vocha mpya ya Airtel Tabasamu ambayo ni maalumu kwa wateja wake wa malipo ya awali nchini. (kushoto) Meneja wa chapa wa Airtel , Arnold Madale na Meneja Masoko ya Airtel , Anethy Muga (kulia).  Vocha hiyo itapatikana kuanzia sasa kupitia maduka yote ya Airtel , wakala na wachuuzi wa vocha za Airtel nchi nzima.
Meneja Masoko ya Airtel , Anethy Muga( kulia) akiongea wakati wa uzinduzi wa  vocha mpya ya Airtel Tabasamu ambayo ni maalumu kwa wateja  wa Airtel wa malipo ya awali nchini. (kushoto) Meneja wa chapa wa Airtel , Arnold Madale na (katikati) Meneja  Uhusiano wa Airtel , Jackson Mmbando . Vocha hiyo itapatikana kuanzia sasa kupitia maduka yote ya Airtel , wakala na wachuuzi wa vocha za Airtel nchi nzima.

 Airtel wazindua vocha ya kiwango cha chini kabisa kwa wateja wa simu za mkononi  
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imezindua vocha mpya ya muda wa maongezi kwa wateja wake wa malipo ya awali nchini itakayowaongezea wateja wake TABASAMU pale wanapopiga simu au kuitumia kwa matumizi yoyote ya kuwasiliana au kujiunganisha kwenye vifurushi vya gharama nafuu.

Vocha  hiyo mpya ya TABASAMU kwa shilingi 200 inapatikana kwa wachuuzi wote wa vocha za Airtel na kuwawezesha wateja wa Airtel na watanzania wote watakaojiunga na Airtel kumudu gharama za mawasiliano wakati wowote kwa gharama nafuu zaidi

Akiongea wakati wa uzinduzi, Meneja Masoko wa Airtel , Bi Aneth Muga alisema “ Leo tunajisikia fahari kuzindua na kuitambulisha sokoni vocha ya muda wa maongezi ya shilingi 200 itakayowapatia wateja Tabasamu na uhuru wa kuwasiliana na ndugu jamaa marafiki au wale wajasiliamali kuweza kuitumia kupanga mipango yao wakati wowote mahali popote kwa gharama nafuu”

“Tunatambua mawasiliano ya simu ni muhimu katika kuendesha shughuli zetu za kila siku na hivyo  kuboreshwa  kwa viwango vya vocha kutasaidia  sana kuchochea upatikanaji wa huduma ya mawasiliano kwa wote. Tunataka kuendelea kutoa huduma bora za kibunifu na zenye kukidhi mahitaji ya wateja wetu huku tukiwawezesha kutatua changamoto zao za kila siku”. Alieleza Bi,  Muga

“Tunaamini kwa kuwezesha upatikanaji wa vocha za shilingi 200 sokoni tumewawezesha zaidi ya watanzania milioni 10 kuunganishwa na huduma za mawasiliano na kufurahia ofa mbalimbal zinazotolewa na Airtel. Aliongeza muga

Ili kuingia vocha ya muda wa maongezi mteja atapiga *104*  kisha kuingiza namba zilizokwanguliwa na kubonyesha alama ya reli # na kisha OK. Vocha hiyo itaingia moja kwa moja kwenye Salio lake la kupiga simu na mteja ataamua kuitumia kwa kupiga simu au kujiunga na kifurushi  cha shilingi 200 kwa kupiga *149*99#.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages