WALIMU NA ASASI ZA KIRAIA WAJENGEWA UWEZO KUHAMASISHA UKUSANYAJI WA RASILIMALI ZA NDANI KUBORESHA SEKTA YA ELIMU - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

WALIMU NA ASASI ZA KIRAIA WAJENGEWA UWEZO KUHAMASISHA UKUSANYAJI WA RASILIMALI ZA NDANI KUBORESHA SEKTA YA ELIMU



Afisa Mradi wa Elimu kutoka TENMET, Bi. Alistidia Kamugisha akielezea juu ya uhusiano wa ukusanyaji kodi na maendeleo katika sekta ya elimu kwenye mafunzo ili kutafuta ufumbuzi wa changamoto za utoaji wa elimu bora hapa nchini mkutano huu umewakutanisha wanachama wa chama cha walimu Tanzania (CWT/TTU) na wadau wa elimu katika mkoa wa Singida.
Mkufunzi wa Mafunzo, Wakili Dominic Nduguru akitoa mada ya uhusiano wa Makusanyo ya Kodi Na Maendeleo ya Sekta ya Elimu kwa baadhi ya wadau na mbalimbali wa elimu mkoani Singida leo kwenye mkutano ulioandaliwa na TENMET wakishirikiana na ActionAid Tanzania.
Meneja Mradi Wa Elimu ActionAid Tanzania, Karoli Kadeghe akichangia mada wakati wa Mafunzo ya wanachama na viongozi wa Chama cha Walimu na Asasi za Kiraia waliokutana mkoani Singida leo.
Mwenyekiti wa Chama cha Walimu Mkoa wa Singida, Bw. Aran Jumbe akielezea hali ya elimu mkoani Singida na namna ambavyo uwekezaji wa Elimu ni muhimu kuinua Sekta ya Elimu hapa nchini Tanzania.
Baadhi ya wadau mbalimbali wa elimu mkoani Singida wakifuatilia mafunzo 
Washiriki wakijadili juu ya upotevu wa kodi nchini kwenye mafunzo yaliyowakutanisha wadau mbalimbali jijini Dar es Salaam.
Picha ya Pamoja

Katika kuzitafutia ufumbuzi changamoto za utoaji wa elimu bora hapa nchini leo Mtandao wa Elimu Tanzania (TENMET) wakishirikiana na ActionAid Tanzania wameandaa mkutano uliowakutanisha wanachama wa chama cha walimu Tanzania (CWT/TTU) na wadau wa elimu katika mkoa wa Singida kwa siku tatu ili kupanga mpango kazi wa utetezi na ushawishi wa masuala ya elimu yatakayoleta matokeo chanya kwenye masuala ya elimu hapa nchini.

Mkutano huu  ulikuwa ulingazia changamoto zinazoikabili elimu ya msingi hapa nchini ikiwemo upungufu wa vyumba vya madarasa, upungufu wa ofisi za walimu, upungufu wa vyoo vya wanafunzi, uwiano usiokubalika kitaratibu wa mwalimu na wanafunzi, shule nyingine kukosa kabisa mwalimu wa kike, upungufu wa nyumba za walimu, kutokutosha kwa fedha za ruzuku, utegemezi wa bajeti ya nchi unaoathiri pia bajeti ya elimu na kusababisha Serikali kushindwa kugharimia kiufanisi utoaji wa elimu.

Mgawanyo wa ruzuku usiozingatia mahitaji ya wenye uhitaji maalumu, jinsia na mahitaji ya kijiografia na pia shule changa na zile ambazo ni kongwe. Kuwa na mipango ya kibaguzi kwa shule inayofanya vizuri ndiyo inapewa fedha (payment for results- P4R) kutoka mpango wa BRN bila kujali mizania ya usawa wa mazingira kati ya shule na shule. Kukosekana kwa mafunzo kazini kwa walimu, kutopandishwa madaraja walimu na utolipwa kwa wakati stahiki za walimu wanaohamishwa/kustaafu mfano pesa ya usafiri.

Katika majadiliano washiriki walichangia juu Upotevu wa kodi nchini hususani katika sekta ya madini na viwanda ndio chanzo cha kukosa fedha za kutosha kugharimia sekta ya elimu nchini. 
Akizungumza leo Afisa Mradi wa Elimu kutoka TENMET, Bi. Alistidia Kamugisha aliwasisitiza serikali kuimarisha vyanzo vya mapato yetu kama nchi hasa kwa kukusanya kodi stahiki kwa kila mtu anayepaswa kulipa kodi. Ili tuondokane na utegemezi toka kwa wahisani. Kwa bajeti ya elimu 2016/17 takribani bilioni 277 sawa na asilimia 31% ilitarajiwa kukusanywa kutoka kwa wahisani na washirika wa maendeleo. Hata hivyo hadi kufikia mwezi Machi 2017 wahisani walikuwa wametoa kiasi cha shilingi bilioni 132 tu, sawa na asilimia 47.6%. 

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Walimu Mkoa wa Singida, Bw. Aran Jumbe  alisema ni vyema serikali iimarishe  vyanzo vyake vya mapato vya ndani, ili kuepuka aibu hii, na pia walisisitizwa wadau wa elimu wanalo jukumu la kuisimamia serikali katika kutimiza wajibu wake. Kila mtu akilipa kodi stahiki kadri ya kile anachozalisha na pia serikali ikidhibiti mianya ya upotevu wa kodi, hata kodi ya PAYE itapungua na kumpa mwalimu ahueni katika makato hayo.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages