Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) umepokea kwa majonzi na masikitiko makubwa taarifa ya vifo vya watu 36 ambao ni wanafunzi 33, walimu wawili na dereva wa gari la shule ya msingi Lucky Vicent ya Arusha vilivyotokea jana tarehe 6 Mei 2017 katika ajali ya gari katika eneo la Rhotia Marera Wilayani Karatu, Arusha.
Katibu Mkuu wa UWT Ndg Amina Makilagi ametoa salamu za pole na rambi rambi kwa familia, wazazi, ndugu na walezi waliopoteza wapendwa wao hasa watoto wadogo waliokuwa wakilelewa kuwa raia wema na nguvu kazi bora ya Taifa letu hapo baadae.
Katika salamu zake Ndg Makilagi amesema UWT inaungana na wanawake, wazazi na waombolezaji wote nchini kuwaombea majeruhi kupona haraka na kumuomba Mwenyezi Mungu aziweke roho za marehemu mahala pema peponi. Amina
Imetolewa na:-
AMINA MAKILAGI
KATIBU MKUU WA UMOJA WA WANAWAKE TANZANIA
07/05/2017.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)