Chemba ya Wafanya biashara, Viwanda na Kilimo ( TCCIA ) imeingia makubaliano na Chemba ya Biashara ya Uturuki (TOBB) mjini Instanbul.TOBB ni chemba ya 2 kwa ukubwa duniani ikiwa na wanachama zaudi ya 1,500,000. Ikumbukwe kuwa Uturuki ni Nchi ya 16 kwa uchumi duniani na kilimo ni Nchi ya 7.
Makubaliano haya yanafuatia Ziara ya Rais wa Uturuki Nchi Tanzania. Ambapo TCCIA na TOBB zimekubaliana kushirikiana kwenye kubadilishana ujuzi, uwekezaji wa pamoja na kukuza biashara .
Pia TCCIA imefungua ofisi yake ya uwakilishi jijini Instanbul ili kukuza biashara kati ya Nchi mbili hizi. Ofisi ya diaspora hii utaongozwa kwa muda na Dr. Miraji.
Zoezi la kutiliana mkataba na TOBB liliongozwa na Makamu Rais wa TCCIA Bw. Octa Mshiu akiongozana na Mshauri wa TCCIA Imani Kajula. Kabla ya kwenda Uturuki ziara hiyo ilianzia Nchini Italy.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)