Mkazi wa Mwanza aibuka na mamilioni ya Biko - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Mkazi wa Mwanza aibuka na mamilioni ya Biko

Msanii nyota wa filamu Tanzania, ambaye pia ni balozi wa Biko, Kajala Masanja, akionyesha namba ya ushindi wa Sh Milioni 10 aliyoshinda mkazi wa Mwanza, Pildas Emmanuel katika mchezo wa kubahatisha unaoendeshwa na Kampuni ya Biko Tanzania. Droo hiyo ilichezeshwa jana, jijini Dar es Salaam. Picha na Mpiga Picha Wetu.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

MKAZI 
wa Mwanza, Pildas Emmanuel ameibuka na ushindi mnono wa Sh Milioni 10 kutoka 
kwenye shindano la ‘Ijue Nguvu ya Buku’ katika droo iliyochezeshwa jana jijini 
Dar es Salaam na kushuhudiwa pia na msimamizi wa Bodi ya Michezo ya 
Kubahatisha Tanzania, Abdallah Hemed.


Droo ya 
bahati nasibu hiyo inayoendeshwa kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi katika 
simu za mikononi kupitia huduma za Tigo Pesa, Airtel Money na M-Pesa ambapo pia 
ilichezeshwa na Balozi wa Biko Tanzania, Kajala Masanja.


Akizungumza 
jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Biko Tanzania, Charles Mgeta, alisema 
kwamba droo hiyo imeshirikisha washiriki zaidi ya 10,000 Tanzania nzima na 
kufanikiwa Emmanuel kutoka Mwanza kunyakua fedha hizo na kuingia katika 
historia ya mshindi wa kwanza kutoka mkoani.


Alisema 
Biko wamefurahia kuona mshindi wa droo ya tatu ametoka mkoani, baada ya droo 
mbili za awali ambazo zote washindi wake walitoka jijini Dar es Salaam kwa 
Christopher Mgaya na Nichoulas Mlasu kuibuka na Milioni 10.


“Tunawapongeza 
washiriki wote wanaogombania gurudumu la mchezo wetu wa Biko ambao umeshika 
kasi, huku nikimpongeza pia mshindi wetu wa mkoani Mwanza, Emmanuel kuibuka na 
ushindi huu ambao kwa hakika unaweza kubadilisha maisha yake.


“Bado 
kila mtu anaweza kuibuka na ushindi wa Sh Milioni 10 kwa droo ya wiki pamoja na 
zawadi za papo kwa papo kuanzia Sh 5000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000 
500,000 na Milioni moja kwa kucheza Biko mara nyingi zaidi kwa kufanya miamala 
kwenye simu zao za mikononi huku namba yetu ya kampuni ikiwa ni 505050 na namba 
ya kumbukumbu ni 2456,” Alisema.


Naye 
Emmanuel alisema bado haamini ametangazwa kushinda zawadi hiyo inayoweza 
kumfanya atimiz ndoto zake za kimaisha kwa kuhakikisha kwamba fedha hizo
anazitumia vizuri endapo atakabidhiwa kutoka Biko,  huku akikiri kuwa ametokea 
kuupenda mchezo wa Biko.


“Nimekuwa 
nikicheza Biko kwa sababu ni mchezo mzuri maana hauna mlolongo mrefu, hivyo 
wakati nasubiria zawadi yangu kutoka Biko, nawashauri Watanzania wote 
kugombania gurudumu la Biko kwa sababu kila mtu anaweza kushinda donge nono,” 
Alisema.


Baada 
ya kutangazwa kunyakua Sh Milioni 10, mshindi huyo anatarajiwa kukabidhiwa 
fedha zake mapema wiki hii kwa utaratibu wa kufunguliwa akaunti katika benki ya 
NMB sambamba na kupewa elimu ya kifedha kama walivyopatiwa washindi wenzake wa 
jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages