Pages

Kanuni uendeshaji mitandao ya kijamii kukamilika mapema- Dk Mwakyembe

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe akizungumza kwenye kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari 2017 linalofanyika jijini Mwanza juzi.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (kulia) pamoja na meza kuu kwenye maadhimisho hayo akizinduwa taarifa ya "So This Is Democracy" ya MISA TAN kwenye maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani zilizofanyika kitaifa mkoani Mwanza juzi. Anaye msadia kushoto ni mmoja wa wajumbe wa bodi ya MISA TAN.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe pamoja na viongozi mbalimbali waliopo meza kuu wakionesha baadhi ya nakala za taarifa ya "So This Is Democracy" ya MISA TAN mara baada ya kuzinduliwa kwenye maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani zilizofanyika kitaifa mkoani Mwanza juzi.

Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika-Tanzania, Salome Kitomari akizungumza kabla ya kumkaribisha Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Mwakyembe kuzungumza kwenye kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari 2017 linalofanyika jijini Mwanza juzi.

Mwanachama wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Valerie Msoka ambaye pia aliwahi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa chama hicho akizungumza kuwasilisha ujumbe wa TAMWA kwenye kongamano hilo la Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari 2017 linalofanyika jijini Mwanza juzi.

Mwakilishi wa Shirika la Mipango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Tanzania, Alvaro Rodriguez akizungumza katika kadamnasi hiyo.

Mtaalamu wa Mawasiliano nchini, Innocent Mungy akizungumza kwenye kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari 2017 linalofanyika jijini Mwanza juzi.
WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe amesema wizara hiyo inaharakisha kukamilisha kwa kanuni zitakazo simamia mitandao ya kijamii inayoendesha shughuli zake kama vyombo vya habari vya kieletroniki (Tv na Redio).
Waziri Dk. Mwakyembe aliyasema hayo jana alipokuwa akizungumza na wadau mbalimbali wa vyombo vya habari na wanataaluma wa vyombo vya habari katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani zilizofanyika kitaifa mkoani Mwanza.
"Hii media nyingine hii ambayo inafanya kazi zilezile kama za vyombo vya habari vya eletroniki, lakini nadhani tulikuwa hatujaamka kutunga kanuni, lakini nauhakika ndani ya muda si mrefu hilo litafanyika...lakini litakuwa zoezi shirikishi kama nilivyo ahidi...," alisema Waziri Dk. Mwakyembe.
Hata hivyo aliwataka wananchi kutumia taarifa za kwenye mitandao kwa tahadhari na kama tetesi ili kuondoa mikanganyiko ambayo imekuwa ikitokea kwenye mitandao hiyo.
Kwa upande wake Mtaalamu wa Mawasiliano, Innocent Mungy akiwasilisha mada ya 'Mchango wa Mitandao ya Kijamii katika kukuza Uhuru wa Kujieleza' kwenye kongamano hilo ilisema mitandao ya kijamii kupitia intaneti imeleta mapinduzi makubwa katika sekta ya mawasiliano licha ya uwepo wa changamoto zake.
Alisema mitandao kama blogu imekuwa ikisambaza taarifa kwa kiasi kikubwa na kutumiwa na idadi kubwa ya watu nchini katika kupata taarifa. "Bloggers wamekuwa sehemu kubwa ya mawasiliano...hadi taasisi mbalimbali zimeona umuhimu wake nazo zimeingia na kuwa zikitumia mitandao hiyo katika kutoa taarifa...," alisema mtaalamu huyo wa mawasiliano nchini.
Akifafanua alisema kutokana na wimbi la kukua kwa mitandao hiyo na kusambaza taarifa wakati mwingine imekuwa vyanzo vya taarifa hata katika vyombo rasmi vya habari. Alisema licha ya mafanikio hayo mitandao hiyo imekuwa na changamoto kubwa ikiwepo uwepo wa taarifa za uongo kupitia mitandao hiyo, matumizi mabaya ya mitandao hiyo.
Aidha akijibu moja ya swali lililoulizwa na Mwenyekiti wa Umoja wa Wamiliki wa Mitandao ya Kijamii (TBN) juu ya mvutano wa mitandao ya kijamii 'Blogu' na vyombo rasmi vya habari kuchukuliana taarifa basipo utaratibu kwa pande zote, alizitaka pande zote kukaa na kuzungumza kwa pamoja kuangalia namna zinaweza kutatua mvutano huo wa chini chini kwa maendeleo zaidi ya tasnia.
"...Nianze kwa kupongeza kuwa kwa sasa bloga wanavyofanya kazi kunamabadiliko makubwa ukilinganisha na hapo nyumba, sasa hivi hadi wao (bloggers) wanaumoja wao unaowaunganisha (TBN). Kaeni chini mzungumze naamini mtayamaliza, mnaweza kuwatumia hata waandishi wa habari wakongwe na hata bloga wazoefu ili kumaliza mgogoro huo wa chini chini na vyumba vya habari," alisema.
Hata hivyo alisema kuwa mitandao ya kijamii sio mibala bali watumiaji wake ndio wabaya na kuongeza mitandao hiyo imekuja na mabadiliko makubwa katika sekta ya mawasiliano.

Baadhi ya wanataaluma ya habari na wadau anuai wa vyombo vya habari wakiwa kwenye kwenye kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari 2017 linalofanyika jijini Mwanza.

Moja ya kikundi cha burudani kikitoa burudani katika maadhimisho hayo.

Moja ya kikundi cha burudani kikitoa burudani katika maadhimisho hayo.

Afisa Habari na Utafiti kutoka Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania, Gasirigwa Sengiyumva, akizungumza kwenye kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari 2017 linalofanyika jijini Mwanza juzi.

Baadhi ya wanataaluma ya habari na wadau anuai wa vyombo vya habari wakiwa kwenye kwenye kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari 2017 linalofanyika jijini Mwanza.

Baadhi ya wanataaluma ya habari na wadau anuai wa vyombo vya habari wakiwa kwenye kwenye kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari 2017 linalofanyika jijini Mwanza.

Mwenyekiti wa TEF, Theophil Makunga akiwasilisha ujumbe kutoka TEF Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari 2017.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)