Mkuu wa mkoa wa Arusha, Bw Mrisho Gambo akiwa pamoja na wazazi wa majeruhi wa ajali ya wanafunzi wa Lucky vicent katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa KIA kabla ya safari ya kuelekea Marekani kwaajili ya matibabu yaliyotolewa na taasisi ya Samaritan's Purse, Ajali hiyo iliyotokea wiki iliyopita huko Karatu na kupoteza maisha ya Wanafunzi, walimu na dereva kufikia 34
Majeruhi watatu wa ajali ya basi la wanafunzi la Lucky Vicent wakipakiwa kwenye Ndege ya Taasisi ya Samaritan's Purse ambao wamejitolea kuwahudumia kwa matibabu majeruhi hao kwa kuwasafirisha nchini Marekani kwa Matibabu zaidi huku majeruhi hao wakiongozana na wazazi wao, daktari mmoja na nesi mmoja kwa kila majeruhi
Ndege ya Taasisi ya Samaritan's Purse ikiwa katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro mapema leo asubuhi tayari kwa kuruka mpaka Marekani kwaajili ya kuwapeleka majeruhi wa ajali ya basi la wanafunzi wa Lucky vicent iliyotokea wiki iliyopita na kupoteza watu 34 huko Karatu.
Sehemu ya ndani ya Ndege ya Samaritan's Purse iliyowabeba majeruhi watatu wa ajali ya wanafunzi wa shule ya Lucky Vicent ambao leo wamesafirishwa kuelekea nchini Marekani kwaajili ya matibabu zaidi huku gharama za matibabu hayo yakitolewa na taasisi ya Sammaritan's Purse.
Baadhi ya wananchi, ndugu jamaa na wakazi wa Mkoa wa Kilimanjaro na Arusha waliojitokeza kwaajili ya kuwasidikiza majeruhi watatu wa ajali ya basi la wanafunzi wa Lucky Vicent iliyotokea wiki iliyopita huko Karatu Arusha Tanzania.Picha kwa Msaada wa Mtandao wa Whatsapp.
Majeruhi watatu wa ajali ya basi la wanafunzi la lucky Vicent iliyotokea wiki iliyopita wilayani Karatu Mkoani Arusha na kupoteza watu takribani 34 leo wamesafirishwa na Ndege ya taasisi ya Samaritan's Purse kuelekea nchini Marekani kwaajili ya kupatiwa matibabu zaidi kutokana na majeraha waliyoyapata kutokana na ajali hiyo iliyopelekea kupoteza maisha ya wenzao 30, dereva 1 na walimu wawili.
Majeruhi hao ambao ni Doreen Mshana (13), Sadia Ismael Awadhi (11) na Wilson Geofrey Tarimo (11) wameongoza na wazazi wao huku kila mmoja akiwa na usaidizi wa daktari mmoja na nesi mmoja kutoka hospitali ya Mount Meru Arusha.
Lukaza Blog inapenda kuwatakia safari njema ya matibabu yao Na Mungu akapate kuwaponya haraka ili kusudi wareje kuendelea na maandili ya mtihani wao wa taifa wa Darasa la Saba.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)