SHEREHE za Sikukuu ya Muungano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, zimetumika kama sehemu ya kutangaza utalii wa Tanzania katika tukio maalum lililoandaliwa na Ubalozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wan chi hiyo.

Akizungumza hivi karibuni katika sherehe hizo za Sikukuu ya Muungano wa Tanzania, Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, H.E Hemed Mgaza, alisema kwamba Tanzania ni eneo zuri la uwekezaji kutokana na sera zake nzuri pamoja na dhamira njema za viongozi chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr John Pombe Magufuli kwa Tanzania Bara pamoja na Dr Ali Mohamed Shein kwa upande wa Visiwani Zanzibar.