Maofisa waandamizi wa TBL Group wakiwa wameshilia vikombe vya tuzo za ushindi
Makamu wa Rais,Mh. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza kwa makini Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group Deogratius ( wa pili kushoto) wakati alipotembelea banda la kampuni hiyo wakati wakati wa utoaji wa Tuzo za Rais za mzalishaji bora wa Viwanda kwa mwaka 2016 katika hoteli ya Serena mwishoni mwa wiki.Kulia ni Waziri wa Viwanda ,Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage na kushoto ni Afisa Masuala Endelevu wa TBL Group, Irene Mutiganzi.
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan (kushoto) akimkabidhi Tuzo ya mshindi wa jumla ya mzalishaji bora wa viwanda mwaka 2016 Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group Deois Deogratius wakati wa hafla tuzo hizo iliyoandaliwa na Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania( CTI) na kufanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan (kushoto) akimkabidhi Tuzo ya mshindi ya mzalishaji bora wa viwanda mwaka 2016 Meneja wa Kiwanda cha TBL jijini Dar es Salaam,Calvin Martin, wakati wa hafla tuzo hizo iliyoandaliwa na Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania( CTI) jijini Dar es salaam.
Meneja wa bia ya asili ya Chibuka Super inachozalishwa na TBL Group , Fredy Kazindogo (kushoto) akimuonyesha Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan chupa ya Chibuku iliyotengenezwa kwa ubora wakati banda la TBL Group.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh. Samia Suluhu Hassan akingalia bidhaa zinazozalishwa na kampuni ya TBL Group
Wafanyakazi wa TBL Group katika picha ya pamoja muda mfupi baada ya kampuni yao kuibuka kidedea
Kampuni ya TBL Group imeibuka tena na ushindi wa jumla wa tuzo ya Rais ya mzalishaji bora kwa mwaka 2016.Imefanikiwa kuweka rekodi ya mwendelezo ya ushindi ambapo pia mwaka jana iliibuka kuwa mshindi wa jumla wa tuzo hii.
Tuzo ya mzalishaji bora hutolewa na Chama Cha Wenye Viwanda Tanzania (CTI) na hafla ya kukabidhi tuzo kwa washindi mbalimbali ilifanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki ambapo mgeni wa heshima aliyekabidhi tuzo alikuwa ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh. Mh.Samia Suluhu Hassan.
Mh.Samia Suluhu Hassan, aliahidi kuwa serikali itazifanyia kazi haraka changamoto zinazokabili wafanyabiashara wenye viwanda ili kufanikisha dhamira yake ya kujenga Tanzania ya Viwanda.
TBL ni kampuni ya kwanza kutengeneza vinywaji vyenye kilevi nchini.Mbali na tuzo ya mzalishaji bora inashikilia pia rekodi ya tuzo ya mwajiri bora nchini. Mafanikio haya yanatokana na uwekezaji mkubwa uliofanywa kwenye mifumo ya uzalishaji,raslimali watu na kunufaisha jamii kupitia mzunguko wa biashara zake ambao umefanikisha kupatika ajira zipatazo 2,000 za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja .
Kampuni pia imekuwa mstari wa mbele kuchangia maendeleo ya taifa kupitia kulipa na kukusanya kodi za serikali ambapo pia inashikilia tuzo mbalimbali kwa kuwa mlipa kodi bora nchini.
Mbali na kushinda Tuzo ya mzalishaji bora kwa mwaka huu pia imefanikiwa kutunukiwa tuzo ya kuwa kiwanda bora cha vinywaji nchini na tuzo ya matumizi mazuri ya nishati katika mchakato wa uzalishaji-Tuzo hizi zinazidi kudhihirisha umakini wa TBL Group katika uwekezaji wake ambapo pia inashikilia tuzo ya kimataifa ya mwajiri bora iliyotunikiwa mwaka jana na taasisi ya Top Employers’ Institute yenye makao yake makuu nchini Uholanzi kutokana na kuwa miongoni mwa makampuni yanayozingatia kanuni bora za raslimali watu katika viwanda vyake duniani.
Akiongea baada ya hafla ya kupokea tuzo,Meneja wa kampuni ya TDL ambayo iko chini ya TBL Group,Devis Deogratius alisema “Ushindi huu wa TBL mfululizo unadhihirisha kuwa Tanzania ya Viwanda bora inawezekana na mbali na ushindi huu viwanda vyetu vya bia vya Mwanza, Mbeya, Arusha na Dar es Salaam vinashikilia rekodi ya kushinda tuzo za kuwa miongoni mwa viwanda bora barani Afrika na duniani.”
Deogratius alisema kipaumbele kikuu ambacho kampuni inazingatia ni kuhakikisha inazalisha bidhaa zenye ubora wa hali ya juu na kwa upande wa vinywaji vyenye kilevi imekuwa mstari wa mbele kuelimisha jamii juu ya unywaji wa kistaarabu na ni miongoni mwa makampuni yanayotekeleza maazimio ya mkutano wa kidunia wa watendaji wakuu wa makampuni yanayotengeneza vinywaji vyenye kilevi kuhusiana na kutoa elimu ya Unywaji wa kistaarabu kwa watumiaji wa vinywaji vyenye kilevi.
Mafanikio haya yote yanaifanya TBL kuendelea kuaminika kwa wengi kama kampuni halisi ya kitanzania inayotengeneza bia bora kwa kutumia malighafi kutoka nchini ambazo licha ya kupendwa na wananchi wengi zinakubalika kwenye masoko ya nje na zimetunikiwa tuzo mbalimbali za kimataifa za ubora.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)