Ndugu, jamaa na marafiki hii leo jumatano April 05,2017 wameuaga mwili wa marehemu Profesa Lloyd Manamba Binagi aliyefariki ghafla juzi jumatatu April 03,2017 Jijini Dar es salaam, kwa ajili ya kusafirishwa kwenda mkoani Mara kwa ajili ya mazishi.
Mwili huo utapokelewa kesho asubuhi katika uwanja wa ndege Jijini Mwanza, na baadaye kusafirishwa kwenda nyumbani kwa marehemu Bomani wilayani Tarime.
Mazishi yanatarajiwa kufanyika katika malalo ya Binagi yaliyopo Kenyamanyori wilayani Tarime siku ya jumapili, April 09,2017 baada ya familia ya marehemu kuwa imewasili kutoka nchini Marekani.
Bwana alitoa, Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe, Amina!
Picha na Msubi BMG
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)