Pages

Mvua yaleta Songombingo Bukoba Mjini.Nyumba zageuka Mabwawa

Mvua kubwa imeendelea kunyesha leo Jumamosi April 8,2017 na kusababisha athari kwa wakazi wa Mji wa Bukoba,pichani wanaonekana wananchi wakipata usumbufu katika daraja la Kanoni kutoka eneo moja kwenda jingine.
Magari yaliyo egesha nayo yamepatwa na dhahama hii 
 Muonekano wa bango linalotoa angalizo kwa watu kujenga maeneo hayo
 Darajani Kanoni wananchi wakipata tabu kuvuka, mpaka tunaingia mtamboni hatujajua ni kiazi gani cha athari iliyojitokeza .
 Hali ilivyo mtaa wa Omkigusha Manispaa Bukoba.
 Kiota Cha Sky motel Bukoba kikiwa kimezingirwa na Maji kufuatia mvua kubwa ilionyesha leo
 Wananchi wakitazama hali ilivyo katika mitaa ya Uswahili Bilele pembezoni mwa Mto kanoni
 Baadhi ya mali zilizo okolewa
Maeneo mbalimbali  Mashuhuda wakifuatilia ili kujionea madhara ya miundombinu yaliyojitokeza
 Mashuhuda yakiangalia hali inavyoendelea kufuatia mvua kubwa iliyonyesha leo Jumamosi Mjini Bukoba
 Mwenyekiti wa Mtaa wa Omkigusha pichani katikati akielezea athari iliyojitokeza kwenye kaya yake
 Baadhi ya wakazi wa Omkigusha wakiwa nje ya nyumba zao zilizoku
Heka heka za wananchi zikiendelea  katikati ya viunga vya bukoba (kashozi road)
 Umati wa watu wakiwa wamekusanyika kushhdia hali ilivyo eneo la Hamgembe darajani.
 Maeneo kandakando ya Mto kanoni Manispaa Bukoba yakiwa yamefurika maji kufuatia mvua iliyonyesha kwa muda mrefu 
 Wenye uwezo wa kuwasaidia wenzao wakifanya kuwajibika kwa kubebana mgongoni.
Baadhi ya wakazi Omkigusha wakiwa juu ya paa na kuta za nyumba zao.
Credit to Bukoba Wadau 

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)