MTU MMOJA AUAWA AKIDHANIWA KUWA NI MWIZI WA PIKIPIKI - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MTU MMOJA AUAWA AKIDHANIWA KUWA NI MWIZI WA PIKIPIKI


Na.Vero Ignatus ,Arusha.


Mtu moja 
ambaye jina lake hajijafahamika ameuawa na wananchi wenye hasira  
kali huko maeneo ya kwa Mrombo Jijini Arusha ,akidhaniwa kuwa ni mwizi 
wa pikipiki baada ya mtu huyo kupita na kufananishwa na waendesha
pikipiki hao.



Kamanda 
wa polisi mkoa wa Arusha Charles Mkumbo amethibitisha kutokea kwa 
tukio hilo  ambapo amesema kuwa  majira ya saa saba mchana 
wananchi hao walimuona mtu huyo wakadania kuwa ndiye aliyewahi 
kumnyanyanya  mwenzao pikipiki hivyo wakaanza kumshambulia na 
kumburuza ambapo hadi jeshi la polisi kufika eneo la tukio mtu huyo
alikuwa tayari ameshachoka na hali yake ilikuwa mbaya wakiwa njiani 
kumpeleka hospitali alifariki.



Kamanda Charles Mkumbo amewataka wananchi kutochukua sheria mkononi kwani wanaweza kumdhuru mtu ambaye hausiki na tukio amesema kuwa wanapomuhisi mtu kuwa ni muhalifu watoe taarifa kwa jeshi la polisi ili sheria ichukue mkondo wake. 



Hadi sasa 
jeshi la polisi mkoani hapa linawashikilia watu watano ambao ni 
waendesha pikipiki kwa kuhusika katika tukio hilo,mwili wa marehemu
umehifadhiwa katika hospitali ya maountmeru ukisubiria ndugu na jamaa 
kwenda kumtambua.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages