MTAMBO WA KISASA WA ED –XRF KWA AJILI YA UCHUNGUZI WA KIMAABARA WAZINDULIWA RASMI MKOANI MBEYA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MTAMBO WA KISASA WA ED –XRF KWA AJILI YA UCHUNGUZI WA KIMAABARA WAZINDULIWA RASMI MKOANI MBEYA


Muonekano wa Picha ya Mtambo wa kisasa wa ED –XRF kwa ajili ya uchunguzi wa kimaabara ambao umezinduliwa  rasmi Mkoani Mbeya.

Na EmanuelMadafa,JamiiMojablog
OFISI ya Mkemia Mkuu wa Serikali, leo imezindua  na kusimika mtambo mpya wa ED-XRF utakao tumika kufanya uchunguzi wa sampuli na vielelezo mbalimbali vikiwemo vya makosa ya jinai.
Akizungumzia Mtambo huo, Mkemia Mkuu wa Serikali, Profesa Samweli Manyele,alisema lengo kuu ni kurahisisha shughuli za kimaabara pamoja na usimamizi wa sheria zilizo chini ya wakala hiyo.
Alisema, baadhi ya kazi zitakazofanywa na maabara hiyo ni kuhakiki ubora na usalama wa bidhaa, sampuli za mazingira, sampuli zinazohusisha makosa ya jinai kama vile sampuli za vinasaba na dawa za kulevya.
“Awali vipimo vya namna hii vilikuwa vikifanyika Jijini Dar es Salaam tu, ofisi za mikoa zilikuwa zikifanya kazi ya kukusanya sampuli na kusafirisha lakini sasa mtambo huu, umesimikwa Mbeya na utatumiwa na Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini kufanya kazi hiyo“alisema  
Amesema maabara ya Mkemia Mkuu wa serikali ni taasisi pekee ambayo inafanya uchunguzi wa vielelezo vya sayansi ya makosa ya iinai ili kusaidia vyombo vya sheria hususani jeshi la polisi na mahakama katika kufanya uchunguzi ili kutoa haki kwa jamii.
“Maabara inachaangia katika kutekeleza sera ya afya ya mwaka 2007 kwa kufanya uchunguzi wa kimaabara kwa kuhakiki ubora na usalama wa bidhaa zinazo zalishwa viwandani “alisema Profesa Manyele.
Amesema maabara ya Mkemia mkuu wa serikali inasimamia utekelezaji wa sheria ya usimamizi wa udhibiti wa kemikali na majumbani sura  182 na sheria ya usimamizi wa teknolojia ya vinasaba vya binadamu sura 732009.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Ndugu Paul Ntinika ametoa wito kwa viwanda ,mashirika wajasiriamali na wananchi kwa ujumla kutumia huduma zinazotolewa na maabara ya mkemia mkuu wa serikali ili kuhakiki ubora wa  bidhaa zinazozalishwa  viwandani.
Mwisho.

Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Paul Ntinika (kushoto) pamoja na Mkemia Mkuu wa Serikali (kulia  aliyeshika utepe Profesa Samwel Manyele  kuashiria uzinduzi rasmi wa mtambo wa kisasa wa ED –XRF ajili ya uchunguzi wa kimaabara mkoani mbeya.

Mkemia Mkuu wa Serikali Profesa Samwel Manyele akizungumza katika uzinduzi rasmi wa mtambo wa kisasa kwenye kikao cha uzinduzi wa mtambo wa kisasa wa ED –XRF kwa ajili ya uchunguzi wa kimaabara ,ambapo hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa hospital ya Mkoa jijini Mbeya.

Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Ndugu Paul Ntinika akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mtambo wa kisasa wa ED –XRF  kwa ajili ya uchunguzi wa kimaabara leo Machi 10 katika hospital ya Mkoa jijini Mbeya.

Wadau kutoka taasisi mbalimbali mkoani mbeya wakiwa katika kikao cha uzinduzi wa mtambo wa kisasa wa ED –XRFkwa ajili ya uchunguzi wa kimaabara.

Meza Kuu katika Picha ya Pamoja na wageni waalikwa.Picha David Nyembe

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages