MBUNGE MSTAAFU WA TEMEKE, ABBAS MTEMVU AFUNGUA MKUTANO WA VICOBA NA BENKI YA KIISLAMU YA AMANA PTA JIJINI DAR ES SALAAM - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MBUNGE MSTAAFU WA TEMEKE, ABBAS MTEMVU AFUNGUA MKUTANO WA VICOBA NA BENKI YA KIISLAMU YA AMANA PTA JIJINI DAR ES SALAAM


Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Kuondoa Umasikini Tanzania (PFT), Mbunge mstaafu wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu (kulia), akibadilishana mawazo na baadhi ya Maofisa wa Benki ya Kiislamu ya Amana, wakati alipofika kwenye ukumbi wa PTA, viwanja vya Sabasaba kuufungua mkutano wa wanachama wa Vicoba wa Wilaya ya Temeke na benki hiyo, mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.(Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Kuondoa Umasikini Tanzania (PFT), Mbunge mstaafu wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu akisalimiana na baadhi ya wanachama wa vikundi mbalimbali vya Vicoba, wilayani Temeke, wakati alipofika kwenye ukumbi wa PTA, viwanja vya Sabasaba kuufungua mkutano wao na Benki ya Kiislamu ya Amana, jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Kuondoa Umasikini Tanzania (PFT), Mbunge mstaafu wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu akimpatia pesa mmoja wa watoto wa wajasiriamali hao, wakati akisalimiana nao ukumbini hapo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Kuondoa Umasikini Tanzania (PFT), Mbunge mstaafu wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu akimpatia pesa mmoja wa watoto wa wanachama wa vikundi hivyo.
Mhe. Abbas Mtemvu akisalimiana na baadhi ya wanachama wa vikundi mbalimbali vya Vicoba, wilayani Temeke, alipofika kwenye ukumbi wa PTA, viwanja vya Sabasaba kufungua mkutano wao na Benki ya Kiislamu ya Amana, jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Maofisa wa Benki ya Kiislamu ya Amana, wakimpokea mgeni rasmi katika ufunguzi wa mkutano wa wanachama wa Vicoba wa Wilaya ya Temeke na benki hiyo, Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Kuondoa Umasikini Tanzania (PFT), Mbunge mstaafu wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu (wa tatu kushoto), alipofika ukumbini hapo, mwishoni mwa wiki.

Baadhi ya wanachama wa vikundi mbalimbali vya Vicoba, wilayani Temeke, wakiwa kwenye ukumbi wa PTA, viwanja vya Sabasaba katika mkutano wao na Benki ya Kiislamu ya Amana, jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wanachama wa vikundi mbalimbali vya Vicoba, wilayani Temeke, wakiwa kwenye ukumbi wa PTA, katika mkutano wao huo na Benki ya Kiislamu ya Amana, jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanachama wa vikundi mbalimbali vya Vicoba, wakiwa katika mkutano huo, ukumbi wa PTA, viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.
Mlezi wa Vicoba, wilayani Temeke, mke wa Mbunge mstaafu wa Temeke, Abbas Mtemvu, Mama Mariam Mtemvu, akiwasalimia wanachama wa vikundi mbalimbali vya vicoba, wakati wa mkutano wao na Benki ya Kiislamu ya Amana, mwishoni mwa wiki.
Mwanachama wa Vicoba, wilayani Temeke, Blandina Makange akisoma risala ya wajasiriamali hao, wakati wa ufunguzi wa mkutano wao huo.
Kaimu Mkurugenzi Mkurugenzi wa Benki ya Kiislamu ya Amana, Muhidin Ally akizungumza na wanachama wa vikundi mbalimbali vya Vicoba, katika mkutano huo. Katikati ni mgeni rasmi wa mkutano huo, Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Kuondoa Umasikini Tanzania (PFT), Mbunge mstaafu wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu na kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha biashara cha benki hiyo, Munir Rajab.

Mlezi wa Vicoba, wilayani Temeke, mke wa Mbunge mstaafu wa Temeke, Abbas Mtemvu, Mama Mariam Mtemvu, akiwa katika mkutano huo.
Mkuu wa Masoko wa benki ya Amana, Dassu Mussa, akizungumza na wanachama wa Vicoba, wakati akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali kuhusu benki hiyo kwa wajasiriamali hao.
Mjasirimali Elina Amani Ngogo, akiuliza swali kuhusu ukopeshwaji wa viwanja vya makazi unaofanywa na benki ya Amana kwa wateja wake, wakati wa mkutano huo.
Mjasirimali Omar Juma, akiuliza swali kuhusu ulipaji wa mikopo ya benki hiyo, baada ya mteja kupata mkopo wake.
Mgeni rasmi Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Kuondoa Umasikini Tanzania (PFT), Mbunge mstaafu wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu akimkaribisha Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Edwin Rutageruka (kushoto), alipofika kwenye mkutano huo.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Edwin Rutageruka (kushoto), akisalimiana na baadhi ya Maofisa wa Benki ya Amana alipofika kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Kuondoa Umasikini Tanzania (PFT), Mbunge mstaafu wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu akizungumza na wanachama wa vikundi mbalimbali vya Vicoba, wilayani Temeke, alipoufungua mkutano wao mwishoni mwa wiki. Kulia ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Edwin Rutageruka na kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha biashara cha benki hiyo, Munir Rajab.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Edwin Rutageruka, akizungumza na wanachama wa vikundi mbalimbali vya Vicoba, wilayani Temeke, wakati wa ufunguzi, wa mkutano wao, ukumbi wa PTA, Sabasaba, jijini Dar es Salaam. Wapili kulia ni Mgeni rasmi Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Kuondoa Umasikini Tanzania (PFT), Mbunge mstaafu wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu, wa pili kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha biashara cha benki ya Amana, Munir Rajab na wa kwanza ni Mkuu wa Masoko wa benki  hiyo, Dassu Mussa.
Meza kuu wakimpigia makofi Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Edwin Rutageruka (hayupo pichani, baada ya kuzungumza na wanavicoba hao.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages