Kufuatia maadhimisho ya wiki ya maji duaniani,
serikali imeunga mkono na kulipongeza shirika la ICS kwa jitihada zake kubwa za
kuhakikisha wananchi wa wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga wanapata maji safi
yanaozalishwa kutoka katika ziwa Victoria. Kamati hiyo ya maji kutoka bungeni
iliongozwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo Mheshimiwa Merry Nagu pamoja na wajumbe
wake 30. Shirika la ICS limekwisha kamilisha mradi huo kwa asilimia 100% na
lipo tayari kuanza kuwanufaisha wananchi wake kwa maji hayo.
Kufuatia mradi huo
kushirikiana bega kwa bega na serikali ya wilaya ya Kishapu, ICS inasubiri
tamko la serikali ambalo linahusisha upangaji wa bei ya maji hayo kutoka EWURA.
Akiwatoa wasiwasi wananchi pamoja na viongozi wa kamati ya bunge ya maji juu ya
uwahishwaji wa bei hio kutoka EWURA, Mhandisi wa Maji wa wilaya ya Kishapu
bwana Lucas Said alisema zoezi hilo lipo katika hatua za mwisho na bei
itatangwa hivi karibuni ili wananchi wanufaike na maji hayo. Hii ni kutokana na
ukweli kwamba pamoja na mradi wa ICS kuwa tayari bado wananchi wanafata maji
umbali mrefu na pia wananunua dumu moja kwa shilingi 500.
Kamati
ya bunge ya maji liadhimia kwa pamoja kuwa kwa kuwa ICS wamekwisha kamilisha
mradi kwa asilimia 100% na bei pendekezi kutoka kwa wananchi na wilaya ya
kishapu kwenda EWURA ni shilingi 30 kwa kila ndoo kinachosubiriwa ni idhini au
maboresho ya EWURA juu ya tamko hilo, Kamati ya bunge imewataka ICS kuanza
kuuza maji kwa shilingi 30 mpaka pale EWURA watakapotoa tamko. Na kuonesha kuwa
kamati hiyo iliazimia kuanza kuwa maji mananchi baadhi ya wanakamati walitoa
kiasi cha fedha na kuwanunulia maji wananchi hivyo zoezi hilo likaanza.
Kufuatia teknolojia itakayotumika katika ununuaji
wa maji hayo kuwa mpya kabisa machonii mwa wanakishapu, Bi Lucy Charles,
mhandisi msaidizi wa Shirika la ICS aliwatoa wasiwasi kwa kuwaeleza kuwa wananchi
watapewa mafunzo ya kutosha ambayo tayari yameshaanza kutolewa ili kila
mwananchi apate maji kwa wakati na bila usumbufu. Maji hayo yatanunuliwa kuwa
mfumo wa Malipo ya Kabla, ambapo kila mwananchi atapewa kadi yake bure, ili
kuweka salio katika kadi hiyo anatakiwa kwenda kwa wakala wa maji ambapo
mawakala hao wanapatikana katika maduka ya kawaida ya bidhaa za nyumbani.
Mwananchi ataweka vocha ya maji kulingana na pesa aliyonayo na pia ataninunua
kulingana na haja yake na salio kama ni kubwa zaidi ya kiasi anachota basi pesa
yake itaendelea kutunzwa katika kadi yake na atakatwa aliyotumia.
Shirika la ICS lenye lengo la kuhakikisha mtoto
na mwanamke wanakuwa katika mazingira salama yatakayoifanya jamii iishi katika
familia zilizo na afya salama, limetumia milioni mia saba hamsini na tano (Tsh 755,000,000) kujenga
mradi wa maji katika vijiji vya Maganzo na Masagala wilayani Kishapu. Shirika
hilo limeyatekeleza hao kwa udhamini mkubwa wa HDIF na UK Aid.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)