Wengi wajitokeza kutoa salamu za mwisho kwa mwili wa Ndugu yetu Jennifer Livigha. - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Wengi wajitokeza kutoa salamu za mwisho kwa mwili wa Ndugu yetu Jennifer Livigha.

Pichani Mpendwa wetu Jennifer Livigha aliyekuwa Mmiliki wa Libeneke la Chinga One na Mwanachama wa TBN Enzi za uhai wake. Marehemu alizaliwa 25.01.1979 Nachingwea, alifariki nyumbani kwake kinyerezi 18.02.2017 Jijini Dar es salaam. Marehemu alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa Ini. Atapumzishwa katika nyumba yake ya milele nyumbani kwao Nachingwea.
 Baadhi ya waombolezaji wakiwa katika Ibada ya kuaga Mwili wa Marehemu Jennifer Livigha aliyekuwa mmiriki wa Blog ya Chinga One katika Hospitali ya Amana.
 Waongozaji wa Ibada ya kuaga mwili wa Marehemu Jennifer
 Waombolezaji wakiwemo baadhi ya wana Tanzania Bloggers Network (TBN) ambapo Marehemu Jennifer alikuwa mwanachama
 Mmoja ya waombolezaji akitoa historia fupi ya Marehemu
Mmoja wa wanafamilia akitoa utaratibu kabla ya kuanza kutoa heshima za Mwisho kwa mpendwa wetu Jennifer
 Baadhi ya wanachama wa Tanzania Bloggers Network (TBN) wakiwa wanaaga mwili wa aliyekuwa mwanachama mwenzao Marehemu Jennifer 'Chinga One'
Baadhi ya ndugu wa karibu, Jamaa na Marafiki wakiwa wanaaga Mwili wa Marehemu Jennifer
Baadhi ya waombolezaji wakiwa wanaimba nyimbo za maombolezo 
Baadhi ya wanachama wa TBN , ndugu, jamaa na marafiki wakiwa wanapeleka mwili wa Marehemu Jennifer katika Gari tayari kwa safari ya kuelekea Nachingwea kwa mazishi
Baadhi ya wanafunzi wakilia kwa uchungu 
Baadhi ya ndugu, jamaa na mafafiki pamoja na wanachama wa TBN wakiwa wanawaaga wanaosafiri na mwili kuelekea Nachingwea
 Mwenyekiti wa TBN Joachim Mushi (Aliyevaa T-Shirt ya Mistari) akiongea jambo kabla ya safari ya kuelekea Nachingwea kwa mazishi.
Baadhi ya wana TBN wakiwa katika Msiba wa mwanachama mwenzao Marehemu Jennifer
 Safari ya kuelekea Nachingwea ikiwa imeanza .. Picha zote  na Fredy Njeje wa TBN

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages