WAZIRI wa Kilimo ,Chakula,Mifugo na Uvuvi Dk. Charles Tizeba (pichani), anatarajia kufungua kongamano la siku tatu la wadau wa sera za kilimo kesho jijini
Dar es Salaam.
Dar es Salaam.
Aidha, kongamano hilo litahudhuriwa na wadau zaidi ya 200 kutoka nchi mbalimbali.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es
Salaam jana, Mwenyekiti wa Kampuni ya Agricultural Non State Actors Forum (ANSAF), Audax Rukonge, alisema serikali imekusudia kuweka kipaumbele kwenye viwanda vya uchakataji wa mazao ya kilimo.
Salaam jana, Mwenyekiti wa Kampuni ya Agricultural Non State Actors Forum (ANSAF), Audax Rukonge, alisema serikali imekusudia kuweka kipaumbele kwenye viwanda vya uchakataji wa mazao ya kilimo.
Kongamano hilo litalenga kuongeza uelewa miongoni mwa watunga sera kuhusu mchango wa kilimo katika kuhamasisha ukuaji wa viwanda Tanzani.
“Wadau watajadili kupata tafsiri halisi ya sekta ya
uchakataji mazao ya kilimo katika muktadha wa mageuzi ya viwanda Tanzania,”alisema
uchakataji mazao ya kilimo katika muktadha wa mageuzi ya viwanda Tanzania,”alisema
Rukonge alisema kongamano hilo limedhaminiwa na USAID, Benki ya Dunia,ANSAF,JICA na wadau wengine ambao wamesaidia kuleta
watalamu wakiwamo wakulima, watafiti,wafanyabiashara na watunga sera.
watalamu wakiwamo wakulima, watafiti,wafanyabiashara na watunga sera.
Mratibu wa Jukwaa la Sera ya Kilimo na Mchumi mwandamizi Wizara ya Kilimo, Sophia Mlote alisema kongamano hilo la tatu litajadili maendeleo ya kilimo nchini ikiwamo kujadili namna ya kutetea sera,sheria,kanuni.
Pia alisema kongamano hilo litajikita katika kujadili juu ya mpango wa kilimo cha mihogo,mikunde, samaki, mazao, usafirishaji pamoja na vifungashio kwa kuwa wazalishaji wengi hawana vifungashio.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)