Meneja wa Kiwanda cha bia cha TBL cha Ilala jijini Dar es Salaam, Calvin Martin,akiongea na wanafunzi hao
Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group,Roberto Jarrin, akiongea na wanafunzi wa Swedish Institute wakati wa ziara yao ya mafunzo katika kiwanda cha TBL cha Ilala
Mmoja wa wanafunzi wa Swedish Instute,Eric Muthomi ,akikabidhi zawadi kwa Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group,Roberto Jarrin kwa niaba ya wenzake
Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group,Roberto Jarrin akibadilishana mawazo na wanafunzi na wakufunzi wa Swedish Institute
Mmoja wa wanafunzi wa Swedish Instute Management Programme Ng’winula Kingamkono akiuliza swali kwa watendaji wa TBL
Wanafunzi kutoka taasisi ya Swedish Institute wakijifunza hatua mbalimbali za uzashaji bia katika kiwanda cha TBL Ilala
-Asema mtazamo wa kampuni yake ni kusonga mbele zaidi katika mchakato wa Tanzania ya viwanda
Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group na Mkuu wa Masoko kanda ya Afrika Mashariki,Roberto jarrin,amesema uanzishwaji wa biashara na uwekezaji unaofanywa kwenye nchi za Afrika unatoa mchango wa kukuza uchumi wa nchi na kuongeza ajira hivyo kuna umuhimu mkubwa kuhakikisha kunakuwepo wataalamu wa kubuni na kuendesha mifumo ya kisasa ya biashara ili biashara hizo zizidi kukua na kuwa endelevu.
Roberto aliyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati akiongea na wafanyakazi kutoka nchi mbalimbali za Kiafrika ambao wanahudhuria mafunzo ya ukuzaji wa biashara endelevu chini ya mpango ujulikanao kama Swedish Institute Management Programme unaolenga kuwajengea uwezo wa biashara na utawala vijana wasomi kutoka barani Afrika walipotembelea kiwanda cha TBL cha Ilala jijini Dar es Salaam.
Alisema biashara yoyote inayoendeshwa kwa kufuata misingi ya kitaalamu ni lazima ipate mafanikio na kuwa endelevu “Biashara ikiendeshwa kwa misingi ya kitaalamu inakua kwa haraka na kuchangua kukuza uchumi wa nchi,kuongeza wigo wa ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja,kuchangia pato kubwa kwa serikali kwa njia ya kulipa kodi na kunufaisha jamii kwa namna mbalimbali”.
Aliwaeleza wanafunzi hao kuwa TBL Group kupitia viwanda vyake vilivyopo kwenye mikoa mbalimbali nchini kwa kiasi kikubwa imekuwa ikizingatia kuendesha shughuli zake kwa kufuata misingi bora ya uendeshaji biashara ambayo kwa kiasi kikubwa imewezesha kampuni kupata mafanikio mengi na kuwa kioo cha uwekezaji bora ambapo watu kutoka sehemu kadhaa wamekuwa wakitembelea viwanda vyake kwa ajili ya kujifunza mifumo ya uzalishaji bora wenye tija na ufanisi.
“Kampuni ya TBL Group imekuwa ikifanya vizuri katika maeneo mbalimbali ikiwemo kuchangia pato la taifa kwa njia ya kulipa kodi,utunzaji wa mazingira,kutoa ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja kupitia mtandao wa biashara zake,kutoa mafunzo ya ujasiriamali kwa wafanyabiashara wadogo inaoshirikiana nao,kuendesha kampeni ya unywaji wa kistaarabu kwenye jamii,kuwezesha wakulima ambao wanaiuzia malighafi na imekuwa kinara wa kutekeleza kanuni bora za ajira ambapo imekuwa ikishikia rekodi ya kupata tuzo ya Mwajiri bora inayotolewa na Chama cha Waajiri nchini (ATE)”.
Roberto alisema kuwa mafanikio haya hayatokani na kufuata mifumo bora ya uzalishaji pekee bali ni kuwa na wafanyakazi wenye vipaji vikubwa na taaluma mbalimbali ambao wanafanya kazi kwa kujituma wakati huohuo kampuni ikiwa inawapatia motisha na mafunzo ya kwa mara ili kuhakikisha wakati wote wanakwenda na wakati sambamba na mabadiliko ya teknolojia yanayotokea siku hadi siku.
Aliwaeleza kuwa TBL Group itaendelea kufanya kazi sambamba na serikali,taasisi zingine na wananchi kwa ujumla kwenye jamii kuhakikisha maendeleo endelevu yanapatikana na aliipongeza taasisi ya Swedish Institute kwa kubuni program ya kuwanoa Vijana wasomi katika mitaala ya uendeshaji biashara kwa mifumo ya kisasa yenye lengo la kuleta ufanisi na kukuza sekta mbalimbali za biashara.
Kwa upande wake Meneja wa mafunzo hayo kutoka taasisi ya Swedish Institute,Matilda Axelsson,alisema ziara ya mafunzo waliyofanya kiwandani hapo imewawezesha wanafunzi wake kupata maarifa kuhusiana na mifumo bora ya uendeshaji wa viwanda kwa tija.
Alisema kuwa taasisi hiyo tangia ianze kutoa mafunzo ya kibiashara na utawala barani Afrika tangia mwaka 2008 imepata mafanikio makubwa ambapo vijana wasomi kutoka nchi mbalimbali wamekuwa wakijiunga kwenye Programu zake za kibiashara kwa ajili ya kunolewa na kuwaanda kuwa waendeshaji wa biashara wazuri “Tutazidi kujipanga kuhakikisha vijana wengi wasomi wanapata fursa za kuhudhuria mafunzo haya na natoa wito kwa waajiri kuwadhamini wafanyakazi wao kupata mafunzo zaidi ili kuleta ufanisi wa kibiashara kupita raslimali watu”.Alisema.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)