Mhe,Jaji Mstaafu wa mahakama kuu kanda ya Arusha Fatuma Hamis Masengi |
Picha ya pamoja kati ya waheshimiwa majaji kanda ya
Arusha na Kilimanjaro ,Wakwanza kulia ni mhe,Jaji Dkt.Modesta
Opiyo,Wakwanza kushosto ni mhe,Jaji Salma Maghimbi,akifuatiwa na
aliyeko kushoto kwake mhe,Jaji Sekela Mushi,akifuatiwa na mhe,Jaji
mstaafu Fatuma Hamis Masengi wakiwa na majaji wengine pamoja na
waheshimiwa mahakamu.Picha na Vero Ignatus Blog.
Mhe,Jaji Mstaafu wa mahakama kuu kanda ya Arusha Fatuma
Hamis Masengi akiwa na waheshimiwa mahakimu wa mahakama ya
mwanzo(waheshimiwa mahakimu hao wamelelewa na mhe,Fatuma
Masengi)
Picha ya pamoja ya waheshimiwa majaji pamoja na mawakili wa serikali,na wale wa kujitegemea.Picha na Vero Ignatus Blog.
Na.Vero Ignatus.
Sherehe ya kumuaga aliyekuwa Jaji mfawidhi wa mahakam kuu kanda ya Arusha Mhe,Fatuma Hamis Masengi ,zimefanyika leo katika mahakama kuu
ya ndanda hiyo na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo
majaji,mahakimu,mawakili wasajili wa mahama watendaji pamoja na wageni waalikwa.
Sherehe hizo zimeanza majira ya saa asubuhi katika mahakama ya wazi
ambapo Jaji Fatuma alianza kufanya kazi mnamo mwaka 1974 katika
mahakama ya mwanzo na kuendelea kuitumikia mahakama hadi alipoteuliwa kuwa jaji mfawidhi mahakama kuu.
Amewataka majaji na mahakimu pamoja na wale wote wanaofanya kazi za kimahakama wafanye kazi kwa kumtegemea Mungu huku wakijua kazi yeyote ina changamoto zake hivyo ni vyema kufanya kazi kwa weledi zaidi na kwa kuzingatia sheria inavyosema,wakimtendea haki kila mtu kwa stahiki.
Amewataka wanawake kutokukata tamaa huku akisema kuwa wanawake wanaweza kuliko wanaume japo kuwa wakati mwingine wanaume wanaona kama vile wanawake ni wanyonge lakini mwanamke anaweza pale ambapo anasimama kwa nafasi yake na kulitumikia kusudi kwa wakati na weledi.
"Wanawake wenzangu msikate tamaa na kujiona wewe ni dhaifu ,tunaweza msibweteke unapopata nafasi itumie vizuri bila kuaharibu taratibu zilizowekwa ,fanya kazi kwa bidii na jamii itaona juhudi zako ,wanawake tunaweza "alisema masengi.
Aidha Jaji Fatuma amesema kuwa anamshukuru sana Mungu kwa kumuwezesha kwa wakati wote ambapo amekuwa akifanya kazi yenye majukumu mazito, amezishukuru Asasi za kiserikali na zile
zisizo za kiserikali,amewashukuru wale wote walioshirikiana nae katika
kipindi chote alichokuwa akitimiza majukumu yake ya
kikazi.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)