Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Bwana, Laurean Bwanakunu (kushoto) na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha Bi.Jenifa Omolo wakibadilishana hati baada ya kusaini makubaliano ya umilikishwaji wa eneo la ardhi, lenye ukubwa wa mita za mraba 400,000 Dar es Salaam leo, ambayo itatumika kwa ajili ya ujenzi wa Kiwanda cha kuzalishia dawa na vifaa tiba Kibaha mkoani Pwani.
Muonekano wa chumba cha mkutano wakati wa hafla hiyo ya kutiliana saini. Pichani ni maofisa kutoka Halmshauri ya Kibaha na MSD.
Ofisa Uhusiano Mkuu wa MSD, Etty Kusiluka, akizungumza wakati akimkaribisha Mkurugenzi wa MSD kuzungumza katika hafla hiyo.
Mkutano ukiendelea.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha, Leonard Mlowe (kulia), akisaini hati hizo za makubaliano.
Picha ya pamoja.
Na Dotto Mwaibale
BOHARI ya Dawa (MSD) pamoja na Halmashauri ya Mji wa Kibaha kwa pamoja leo wamesaini makubaliano ya umilikishwaji wa eneo la ardhi, lenye ukubwa wa mita za mraba 400,000 ambayo itatumika kwa ajili ya ujenzi wa Kiwanda cha kuzalishia dawa na vifaa tiba Kibaha mkoani Pwani.
Hatua iyo ni Utekelezaji wa mradi wauzalishaji dawa wa ushirikiano wa sekta ya umma na sekta binafsi yaani PPP, ambapo Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bwana, Laurean Bwanakunu amesema dhamira ya serikali ya viwanda inawezesha mambo makubwa mawili ambayo ni upatikanaji wa ardhi na kisha kutafuta masoko.
Amesema baada ya hatua hii watatangaza zabuni kwa ajili ya kupata wazalishaji wa dawa na vifaa tiba kama vile maji ya dripu, pamba, gozi na dawa za maji za watoto ambayo itasaidia kupunguza gharama za kuagiza dawa kutoka nje ya nchi, ambapo 85% ya awa na vifaa tiba vinaagizwa kutoka nje ya nchi.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha Bi.Jenifa Omolo eneo hilo lipo karibuna miundombinu ya reli na barabara hivyo itakuwa ni hatua ya kuleta maendeleo kwa mji wa Kibaha.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)