BODI YA SHIRIKA LA POSTA YAWAPIGA CHINI VIONGOZI 2 WAANDAMIZI NA KUWASIMAMISHA 2 - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

BODI YA SHIRIKA LA POSTA YAWAPIGA CHINI VIONGOZI 2 WAANDAMIZI NA KUWASIMAMISHA 2


Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Fortunatus Kapinga, akizungumza wakati akimkaribisha Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika hilo, Dk. Haruni Kondo (katikati), kuzungumza na waandishi wa habari, Makao Makuu ya shirika, Dar es Salaam jana. Kulia ni Kaimu Katibu wa shirika hilo, Zuhura Pinde. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania, Dk. Haruni Kondo (katikati), akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam jana, kuhusu uamuzi wa bodi hiyo, kuwaondoa katika nafasi zao viongozi wanne waandamizi na nafasi zao kuchukuliwa na wafanyakazi wengine kutokana na kile alichokieleza kushindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo kwa ajili ya kuliletea tija shirika hilo, lililotetereka kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ni hujuma kutoka kwa baadhi ya wafanyakazi wake. Kushoto ni Postamasta Mkuu, Fortunatus Kapinga na kulia ni Kaimu Katibu wa Shirika, Zuhura Pinde. 
Mmoja wa wafanyakazi walioteuliwa na Bodi ya Shirika hilo kukaimu moja ya nafasi zilizowazi ya Meneja Mkuu Menejimenti ya Rasilimali za Shirika, Macrice Mbodo (kuli), akiwa katika mkutano huo. Kushoto ni Mkuu wa Idara ya Usalama ya shirika hilo, George Mwamgabe. 
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania. Dk. Haruni Kondo, akizungumza na waandishi wa habari, waki wa mkutano huo. Kushoto ni Postamasta Mkuu, Fortunatus Kapinga.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania, Dk. Haruni Kondo (katikati), akifafanua jambo kwa waandishi wa habari, alipozungumza kuhusu uamuzi wa bodi hiyo, kuwaondoa katika nafasi zao viongozi wanne waandamizi na nafasi zao kuchukuliwa na wafanyakazi wengine kutokana na kile alichokieleza kushindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo kwa ajili ya kuliletea tija shirika hilo, lililotetereka kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ni hujuma kutoka kwa baadhi ya wafanyakazi wake. Kushoto ni Postamasta Mkuu, Fortunatus Kapinga na kulia ni Kaimu Katibu wa Shirika, Zuhura Pinde. 
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania, Dk. Haruni Kondo (kulia), akifafanua jambo katika mkutano huo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania. Dk. Haruni Kondo, akisisitiza jambo, wakati akizungumza na waandishi wa habari, jijini jana kuhusu uamuzi ulifikiwa na bodi hiyo.
Baadhi ya viongozi wa Shirika la Posta Tanzania wakiwa katika mkutano huo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania, Dk. Haruni Kondo (wa pili kulia), akizungumza katika mkutano huo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania, Dk. Haruni Kondo, akijibu maswali ya waandishi wa habari katika mkutano huo.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania, Dk. Haruni Kondo. 
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa kazini wakichukua taarifa hiyo, iliyokuwa ikitolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania, Dk. Haruni Kondo. 
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania, Dk. Haruni Kondo (kulia), akimtambulisha kwa waandishi wa habari, Kaimu Meneja Mkuu Menejimenti ya Rasilimali za Shirika, Macrice Mbodo. 
Kaimu Meneja Mkuu Menejimenti ya Rasilimali za Shirika, Macrice Mbodo, aliyetambulishwa kwa waandishi wa habari. 
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania, Dk. Haruni Kondo, akielezea jambo, wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari katika mkutano huo.
Postamasta Mkuu, Fortunatus Kapinga, akijibu maswali ya waandishi wa habari kuhusu ni jinsi gani wanavyokabiliana na matatizo ya upitishwaji dawa za kulevya kwa mfumo wa vifurushi kwenye shirika hilo.
Taarifa kamili ya bodi hiyo kama ilivyowasilishwa na Mwenyekiti wake, Dk. Haruni Kondo jijini Dar es Salaam jana.

SHIRIKA LA POSTA TANZANIA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI MKUTANO ULIFANYIKA KATIKA UKUMBI WA MIKUTANO WA POSTA HOUSE
TAREHE 25 FEBRUARI, 2017
Kwa kuzingatia maendeleo ya mageuzi makubwa yanayojitokeza katika sekta ya mawasiliano, Shirika la Posta Tanzania kama mtoa huduma kwa umma (Public Postal Operator), linawajibika kuhakikisha kuwa huduma za kisasa zinazozingatia vigezo vya ubora, usalama, uadilifu katika utendaji na uwajibikaji zinawafikia watu wengi zaidi katika maeneo yote ya nchi.

Kwa hivi sasa Bodi ya Wakurugenzi pamoja na Menejimenti imechukua hatua katika maeneo yafuatayo:-

1)   KUPAMBANA NA UHALIFU WA MADAWA YA KULEVYA.
Shirika la Posta Tanzania limechukua hatua kadhaa ili kuhakikisha linashiriki na kuchangia kikamilifu jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano za kupambana na uhalifu, ikiwa ni pamoja na usafirishaji, uuzaji na utumiaji wa madawa ya kulevya, usafirishaji na utakatishaji wa fedha haramu, ugaidi, udanganyifu katika utambulisho pamoja na uhalifu mwingine wa kimtandao wa Kitaifa na Kimataifa.

Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika imedhamiria kuongeza msukumo na kasi ya usimamizi ili kupambana na uhalifu huu ambao una madhara makubwa kwa jamii.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages