MAMLAKA ya Usimamizi wa vyombo vya usafiri wa nchi kavu na Majini (Sumatra) mkoani Tanga kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Kitengo cha Usalama Barabarani wameanza operesheni maalumu kwa madereva wanaozidisha abiria na nauli kwenye mabasi yanayotoka mikoa mbalimbali ikiwemo kanda ya kaskazini.
Hatua inafuatia idadi kubwa ya abiria ambao wanatoka mikoa hiyo kurejea mkoani Tanga na maeneo mengine hivyo baadhi ya mabasi wanapandisha nauli kiholea na kuzidisha abiria.
Hayo yalisemwa na Ofisa Sumatra Mkoani Tanga, Dkt Walukani
Luhamba (Pichani Juu) wakati akizungumza na mtandao huo ambapo alisema waliamua operesheni hiyo ili kuweza kudhibiti masuala hayo ambayo yamekuwa yakiwapa wakati mgumu wananchi wanaotumia vyombo hivyo kwa ajili ya matumizi yao.
Operesheni hiyo inafanyika kwenye maeneo ya Mombo,Korogwe, Mkata na Segera ikiwa ni mkakati wa kuhakikisha wanakabiliana na hali hiyo ili kuweza kuikomesha kwa madereva wenye tabia kama hiyo.
Dkt Walukani alisema katika kuhakikisha wanazibiti operesheni hiyo hivi sasa wanamshikilia dereva wa basi la Hood Issa Kayela (30) linalofanya safari zake kutoka mkoani Arusha kuelekea Mbeya anashikiliwa na Jeshi la Polisi katika kituo cha Mkata wilayani Handeni mkoani Tanga kwa kosa la kuzidisha abiria zaidi ya idadi aliyotakiwa kubeba.
Alilitaja basi hilo lilikuwa na namba za usajili T.779 AVL Scania aina ya Torino lilikuwa likitokea mkoani Arusha kuelekea Mbeya ambapo baada ya kumkamata walimpelekwa mahakamani na baada ya kufika huko akukosa dhamana amerudishwa mahabusu na baade ya wiki mbili anatarajiwa kupandishwa kizimbani.
Akizungumza hatua inayofuata,Dkt Walukani alisema baada ya hapo dereva huyo kukaa kwenye kituo hicho kutokana na kukosa dhamana atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili na ikibainika anamakosa kutokana na sheria za Sumatra atafungwa mwaka mmoja au miwili jela.
“Ukiangalia basi hilo la hood lilikuwa linapaswa kupakia abiria 51 lakini lilipokamatwa eneo la mkata wilayani Handeni lilikuwa na abiri 80 jambo ambalo ni hatari sana “Alisema.
“Kutokana na hali hiyo dereva wa basi hilo alipelekwa mahakamani na alikosa dhamani na hivi sasa anashikiliwa kwenye kituo cha Polisi Mkata kwa ajili ya kufikishwa mahakamani na ikithibitisha ana kosa basi atalazimika kwenda Jela mwaka mmoja au miwili hii itakuwa fundisho kwa madereva wengine wenye tabia kama hii “Alisema.
Dkt Walukani alisema baada ya hapo dereva huyo alikaa kwenye kituo hicho baada ya kukosa dhamana atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili na ikibainika anamakosa kutokana na sheria za Sumatra atafungwa mwaka mmoja au miwili jela.
Naye kwa upande wake, Kamanda wa Kikosi cha Usalama barabarani Mkoani Tanga, Nassoro Sisiwayah alisema operesheni hiyo itakuwa endelevu kwa kufanyika kwenye maeneo mbalimbali mkoani Tanga ikiwemo Mombo, Korogwe, Mkata na Segera lengo kubwa kuhakikisha sheria za usafirishaji zinafuatwa.
Alisema katika operesheni hiyo wanazibiti nauli kwenye mabasi y mikoani ambayo hivi sasa kwa asilimia kubwa watu wengi wanarudi kutoka mikoa ya kaskazini ambapo ulanguzi wa nauli umekuwa ukitumika. Habari kwa hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha Blog
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)