Meneja Uhusian Airtel Tanzania
Jackson Mmbando akizungumza wakati wa kutangaza wachezaji waliochanguliwa
kutokana na michuano ya Airtel Rising Stars na kujiunga na timu za taifa za
vijana ikiwemo Serengeti Boys.
Mkurugenzi wa ufundi wa soka la
vijana TFF Kim Paulsen akizungumza wakati wa kutangaza wachezaji
waliochanguliwa kutokana na michuano ya Airtel Rising Stars na kujiunga na timu
za taifa za vijana ikiwemo Serengeti Boys.
Dar es Salaam, Jumatatu 22 Januari 2017. Baada ya kumalizika kwa kliniki ya wiki moja ya Airtel
Rising Stars mwishoni mwa wiki jana, wavulana 16 wamechanguliwa kujiunga na
timu ya taifa ya Serengeti Boys huku wasichana watatu wakichanguliwa kujiunga
na timu ya taifa ya wanawake - Twiga Stars na wengine 17 kuchagulia kuingia
timu ya wasichana chini ya miaka 17 ya Kilimanjaro Queens.
Akiongea na waandishi wa
habari leo kutangaza majina ya wachezaji hao, Mkurugenzi wa Ufundi TFF Salum
Madadi alisema makocha walikuwa na kibarua kigumu kuchangua wachezaji kwani
wachezaji wote walionyesha vipaji vya hali ya juu sana. Madadi alisema kwa hali
hiyo, ni dhahiri kuwa michuano ya Airtel Rising Stars ambayo ilianzia kwenye
ngazi ya wilaya, uchanguzi dhidi ya wachezaji ulikuwa wakuridhisha.
Tulikuwa na jumla ya wachezaji
65 kwenye kliniki ya Airtel Rising Stars, wavulana 40 na wasichana 25. Ni kweli
kuwa wachezaji wote hawawezi kuchanguliwa kuchezea timu ya taifa, lakini
wachezaji ambao wamebaki tutaendelea kuwatumia kwenye michuano mbali mbali ya
vijana. Pia wengine watachanguliwa na klabu zetu kuchezea timu zao za vijana.
Natoa wito kwa uongozi kuwatumia vizuri vijana hao kwani vipaji wanavyo
wanahitaji uzoefu tu, alisema Madadi.
Mimi kama Mkurugenzi wa Ufundi
wa TFF, nitahakikisha Shirikisho inaengemea kwenye upande wa kukuza timu na
mashindano ya vijana ili kujenga timu bora ya Taifa. Natoa shukrani kwa
Airtel katika mchango wake wa kukuza
soka la vijana hapa nchini. Nina uhakika Airtel itaendelea na mashindano haya
ya Airtel Rising Stars ili kuendelea kuibua vipaji vya vijana wetu, alisema
Madadi.
Tuko kwenye harakati za kuhakikisha tunakuwa
na timu za kudumu za umri wa chini ya miaka ya 14, 17 na 19. Tukifanya hivyo
tutaweza kujenga timu ambayo itafanya vizuri kwenye fainali za michuano ya
AFCON ambayo itafanyika hapa Tanzania kwa mara ya kwanza mwaka 2019, aliongeza
Madadi.
Akiongea juu ya
kuchangua wachezaji, kocha mkuu wa timu ya Serengeti Boys Bakari Shime ambaye
alisimamia kliniki hiyo alisema makocha walichangua wachezaji kulingana na
mahitaji ya sasa ya timu ya Serengeti Boys. Tuliengemea kwenye wachezaji ambao
wanaweza kuelewa na kuendana na mfumo wa mpira wa mashidano na wachezaji wenye
uelewa wa haraka. Kama mnavyojua, timu yetu ya Serengeti imecheza mechi nyingi
za kimataifa kwenye miaka miwili iliyopita na hivyo kupata uzoefu wa kimataifa.
Nia yetu ilikuwa kupata wachezaji wa kuendana na mfumo huo, alisema Shime.
Kwa upande wake,
Meneja Uhusiano Airtel Tanzania Jackson Mmbando aliwapongeza wachezaji
waliochanguliwa kujiunga na timu za taifa. Wachezaji hawa walianza kucheza
michuano ya Airtel Rising Stars tangu ngazi ya wilaya. “ Airtel tunayo furaha
kuweza kuwafanya wachezaji hawa kutimiza ndoto zao za kucheza mpira wa kulipwa.
Kama mnavyojua mpira kwa sasa sio burudani pekee, bali pia ni ajira kwa
wachezaji wengi duniani. Ni hamasa kubwa kuona vijana wakianza kujipatia riziki
zao kutokana na vipaji vyao vya kucheza mpira wa miguu” alisema Mmbando.





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)