Ni jambo la kusisimua kutokana na huruka za vijana kwenye mitandao ya kijamii, hii ni mara baada ya kuona matumizi mabaya ya mitandao kama Facebook,Twitter, Instagram nk yakiongezeka. Vijana wengi wanashindwa kutumia mitandao ya kijamii kwa ajili ya faida yao badala yake wamekuwa wakitumia mitandao hiyo, kutafuta wapenzi,utapeli, umbea, kuanika nyeti zao yaani kuweka picha chafu nk.
Katika video hii Kijana Moses alipata urafiki na msichana ambaye anaitwa “Zaydar” mtandaoni, moses alivutiwa zaidi baada ya kuona picha za mrembo Zaydar kwenye Instagram na ndipo alizidi kukoleza urafiki, kuomba namba na kumtaka awe mpenzi wake, Zaydar hakukataa kwani na yeye alikuwa anatafuta mwanaume wa kumchuna kisawaswa.
Picha alizo kuwa akipost ‘Zaydar’ kwenye mitandao yake ya kijamii hazikuwa zake, alikuwa anaweka picha za warembo wengine ambao ni wazuri zaidi. Hivyo huruka ya moses alijua kuwa msichana anaye wasiliana naye ndiye yule kwenye picha kumbe sio. Timbwili zito ni badaa ya Moses na Zaydar kupanga (apointment) ya kuonana live Dar es salaam – Buguruni – Sokoni … angalia video .. tunaomba Support sanaa ya Tanzania Asante Tunamengi ya kukuelimisha kila wiki.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)