Taarifa kwa vyombo vya habari
Dar es Salaam Januari 12, 2017- Kampuni ya Bia ya Serengeti inapenda kuarifu wateja wake na umma na kwa ujumla kuwa video isiyo na maadili iliyosambaa mtandaoni ikiwa inaonesha msanii akiigiza na kuimba wimbo wenye mahadhi ya taarabu mbele ya bango lenye nembo Serengeti Premiur Lager haihusiani na wala haikusambazwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL)..
Tunapenda kuweka bayana kuwa onesho la msanii huyo halikuidhinishwa na SBL Pia msanii huyo sio sehemu na hajawahi kuwa mmoja wa mawakala wetu wanaotoa huduma za kutangaza bidhaa zetu.
Video hiyo ambayo haikukaa na wala kuzingatia maadili ya sanaa pamoja na maonesho ya wazi inatoa picha mbaya na hata maudhui ya sanaa husika jambo ambalo haliwezi kufanya na taasisi inayohesimika ndani ya jamii kama SBL.
SBL imekuwa mstari wa mbele katika kulinda na kusimamia maadili katika shughuli zake za kijamii ikiwa ni pamoja na kuhamasisha unywaji wa kistaarabu.
Tunauhakikishia umma na wateja wetu kuwa SBL inafanya shughuli zake za kijamii kwa kuangalia mambo yenye tija kwa jamii na sio vinginevyo.
Tunashukuru sana kwa kuendelea kushirikiana nasi
Imetolewa na
Mkurungezi wa Mkurungezi wa Mahusiano
Serengeti Breweries Limited.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)