Mbwa aina ya Boerboel
Na Josephat Lukaza
Boerboel
ni mbwa mwenye umbo kubwa, nguvu na mwenye kujiamini sana kutokana na umbo
lake. Jina la BoerBoel limetokana na neno la Kiafrikana/Kiholanzi lenye maana
ya Farm (Shamba). Neno Boel ni neno la zamani la kiafrikana/kidachi katika
lugha za mbwa Wazungu wanasema slang word for dog.
Kwa
hiyo neno boerboel likatafsiriwa na kuwa Farmer's dog (kwa kiswahili tunaweza
kusema mbwa wa shamba). Kwahiyo basi aina hii ya mbwa Boerboel ni mbwa mwenye
asili ya Afrika Kusini alitengenezwa kwaajili ya kulinda makazi na mashamba ya
makaburu huko afrika Kusini.
Asili
ya mbwa hawa imetokana na mchanganyiko wa mbwa wa asili wa afrika kusini na
wale waliokuja nao makaburu wa kizungu, kifaransa na kidachi nchini afrika
kusini.
Mnamo
mwaka 1652 Jan van Riebeeck's aliwasili Cape town afrika kusini akiwa na mbwa
aina ya "Bullenbijter" kwa kipindi hiko makaburu walikuwa na mbwa
wenye maumbo makubwa , walio imara ambao walifanana na mbwa wa asili
waliopatikana nchini Afrika Kusini.
Mnamo
mwaka 1928 Kampuni ya Mgodi wa Almasi ya De Beers walinunua mbwa aina ya
Bullmastiffs na kumsafirisha hadi Afrika Kusini kwaajili ya ulinzi wa Mgodi
wao. Mbegu hii ikachanganywa na mbegu aina ya Boerboel.
Hapa nikiwa na Mbwa aina ya
Boerboel.
Leo
boerboel wamekuwa ni hobyy na kiwanda kwa Waafrika Kusini na sasa mbwa hawa
wamekuwa wakisafirisha kutoka Afrika Kusini kwaajili ya kupelekwa Sehemu
mbalimbali duniani.
Tabia
za mbwa hawa ni kwamba kwanza wana maumbo makubwa (large size breed), wenye
akili (intelligent), wanaojiamini (confidence), imara (stable), na mbwa hawa
wana adabu yaani obidient kwa kizungu. Mbwa hawa wanaendelea kuwa mbwa wa
ulinzi kwa wakulima wengi wa sasa hivi na nimaarufu sana kwa sababu hiyo katika
jamii za mjini.
Boelboel
ni mbwa mwenye nguvu sana kutokana na asili yake ya kuwa mbwa wa shamba na
kuleta mtafaruku kwa wanyama wakubwa wa afrika walao nyama kama vile Simba na
moja ya sababu ni kwamba wanauwezo mkubwa wa kuwalinda makaburu na watu
wengine.
Mbwa
hawa wanapofugwa wanapaswa kuwa na uangalizi wa hali ya juu sana na kutokana na
asili yake ya ukali, inashauriwa mbwa hawa kufundishwa mafunzo ya adabu na ukali
kwasababu endapo utamuacha na asiwe mkali basi mbwa huyu anaweza kuwa na ukali
wa asili ambao unaweza kuleta madhara makubwa kwa jamii kama kuua,Na sheria ya
Nchini Kwetu Tanzania endapo Mbwa ataweza kusababisha kifo au kuua kabisa basi
sharti mbwa huyo anatakiwa kuuliwa na ikumbukwe mbwa huyu ni mbwa ghali sana
ambapo bei yake hufikia mpaka Randi laki 2 ambazo ni sawa na Shilingi za
Kitanzania zaidi ya Milioni 29.
Angalizo:
Mbwa huyu anapotaka kuvamia ni lazima akurukie kwanza shingo kwaajili ya kuweza
kukudondosha chini na mara anapokurukia huwezi kumzuia kwasababu ni mbwa mwenye
nguvu sana na akikuvamia ni lazima akuue kama hutopata msaada wa haraka kutoka
kwa watu wengine
Huyu
ndio Boerboel...Unaweza kunifuata kwenye instagram kwa jina @lukazablog
facebook Josephat lukaza na Kwa Upatikanaji wa Mbwa hawa na wengine, Mawazo,
Ushauri wasiliana nami kwa Simu namba 0712 390 200 au josephat.lukaza@gmail.com
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)