Na Said Msonga
Lori lililosheheni mahindi lililokuwa likitokea soko la Tandale, Manzese jijini Dar es Salaam limevamia njia inayotumiwa na mabasi yaendayo kasi (DART) na kusababisha msururu wa mabasi mengine kusimama kwa muda katika eneo la Manzese Darajani.
Kwa watumiaji wa barabara ya Morogoro kutoka Ubungo kuelekea katikati ya Jiji mnaombwa kuchukua tahadhari na kwa wenye haraka mnaweza kutumia njia nyingine.
Askari wa usalama barabarani wako eneo la tukio kusaidia kuyapitisha magari lakini kutokana na ufinyu wa njia magari yanapita taratibu sana.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)