Pages

Wakazi wa Maganzo na Masagala wafurahia jaribio la upatikanaji wa maji safi na salama kwenye Makazi yao

 Baadhi ya wakazi wa Maganzo na Masagala wakishuhudia majaribio ya upatikanaji wa maji katika nyumba zao
 Wakazi wa Masagala wakiwa katika foleni ya kusubiria upatikanaji wa maji wakati wa majaribio ya mradi wa usambazaji wa maji katika maeneo yao
Wakazi wa maeneo ya Maganzo na Masagala walipata nafasi ya kushuhudia upatikanaji wa maji katika nyumba zao kwa Mara ya kwanza mradi huu wa maji uliotolewa na ICS Tanzania umewawezeshaji wakazi hao kupata maji safi na salama kwenye nyumba zao.

Yote haya yametokea mara baada ya mradi wa kujenga tanki kubwa la kuhifadhia maji kukamilika na kujazwa maji kutoka kwenye chanzo cha maji  na kuwekwa mabomba na sehemu ya kuchotea maji huku kukiwa na mita za kupima matumizi ya maji katika maeneo hayo, mita hizo zimewekwa na Susteg na kujaribiwa huku wakazi hao wakipata nafasi ya kujionea jinsi ya kuchota maji kwa kutumia kadi za benki  zinazopatikana karibu na maduka yao.

Zoezi la ufunguzi rasmi wa mradi wa usambazaji wa maji utafanyika  mara baada ya vituo 25 vya kuchotea maji kukamilika kwa ujenzi wake mnamo Mwezi Januari mwaka 2017

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)