WAJERUMANI WATENGENEZA FILAMU NDANI YA HIFADHI YA TAIFA YA SERENGETI - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

WAJERUMANI WATENGENEZA FILAMU NDANI YA HIFADHI YA TAIFA YA SERENGETI

Mkurugenzi wa Utalii wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Ibrahim Musa (katikati) akizungumza na Mratibu wa uzalishaji wa filamu wa kampuni ya Polyphon ya nchini Ujerumani,Mona Lessnick alipotembelea eneo la Kogatende jirani na  Mto Mara ambapo kulikuwa kukifanyika shughuli za uchukuaji wa picha za video kwa ajili ya Tamthiliya ya Dream Boat.kulia ni Meneja Mawasiliano wa TANAPA,Pascal Shelutete.
Mkurugenzi wa Utalii wa TANAPA,Ibrahim Musa akizungumza na Mona Lessnick katika eneo la Kogatende ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Mratibu wa uzalishaji wa Filamu wa kampui ya Polyphon Studio,Mona Lessnick (kulia) akiwa na Mpiga picha mkuu wa kampuni hiyo ,Manuel Schroeder na Jorg Gariel  wakati wakizungumza na wanahabari  (hawapo pichani) juu ya tukio la uchukuaji wa picha za video katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Eneo la Kogatende ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ambapo picha za video za sehemu ya Tamthiliya ya Dream Boat zimepigwa hapo.
Moja ya gari lililotumika katika tukio hilo likitoka eneoo la tukio kando ya Mto Mara unopita katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Uchukuaji wa picha za video kando ya Mto Mara ukiendelea.
Magari yakiwa yamebeba sehemu ya vifaa kwa ajili ya uchukuaji wa picha za Video.
Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete akiteta jambo na Mona Lessnick katika eneo la Kogatende ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Mkurugenzi wa Utalii wa TANAPA,Ibrahim Musa( katikati) akisikiliza kwa makini maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Jorg Gabriel walipoktana eneo la Kogatende katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Meneja Mawasiliano wa Tanapa,Pascal Shelutete akisaidia kubeba moja ya Kamera kubwa zilizokuwa zikitumika katika matukio ya uchukuaji wa picha katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Moja ya Kamera kubwa iliyokuwa ikichukua matukio katika upigaji picha wa Tamthiliya ya Dream Boat katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Mkurugenzi wa Utalii akiitizama Kamera ambayo ilikuwa iktumika kupiga picha za matukio mbalimbali wakati wa utengenezaji wa filamu hiyo.
Wataamu wakifunga Kamera katika ndge ndogo ya Shirika la ndege la Costal Airline kwa ajili ya upigaji wa picha za juu . 

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii ,Kanda ya Kaskazini.

SEKTA ya Utalii nchini inatarajia kupiga hatua baada ya wasanii maarufu wa filamu kutoka nchi za nje kuanza kutumia baadhi ya maeneo katika vivutio vya Utalii vilivyoko nchini kuandaa sehemu za tamthiliyaa zao.


Kampuni kubwa ya utengezaji wa filamu ya Polyphon Group  ya Humburg  nchini Ujerumani imekuwa ya kwanza kupiga picha za video za sehemu ya tamthiliya maarufu nchini Ujerumani ya Dream Boat ambayo imekuwa ikiooneshwa katika vituo mbali mbali vya televisheni kwa nchi zinazozugumza lugha ya Kijerumani.

Maeneo ambayo picha za video zimechukuliwa ni pamoja na Kogatende na Lobo ndani ya Hifadhi za Taifa za Serengeti ,huku picha nyingine zikipigwa katika Hifadhi ya taifa ya Arusha pamoja na Pori la akiba Endumeti.


“Tumefanya Sehemu moja ya Tamthiliya yetu Botswana,moja Zambia na nyingine Kenya katika muendelezo wa tamthiliya hii inayooneshwa kwa mika 30 sasa,Sehemu ya mwisho ya muendelezo wa filamu hii iliyochukuliwa Afrika ilikua mwa 2007,ni muda mrefu na tuliangalia wapi tunaweza enda,na tukafanya utafiti ,tukaja Tanzania,Tumeona hii nchi ni nzuri tukaamua kuleta filamu yetu hapa”.alisema Manuel Schroeder mpiga picha wa kampuni ya Polyphon Studio.

Mkurugenzi wa Utalii wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Ibrahim Musa amesema hatua hii ni fursa nyingine muhimu kwa Tanzania  kutangaza vivutio vya utalii kimataifa huku mratibu wa uzalishaji wa filamu wa kampuni ya Polyphon,Mona Lessnick akieleza utalii utaongezeka kupitia tamthiliya hiyo.


“Kutokana na uzoefu ,watu wametuamini sisi , tumefanya hii kazi kwa miaka 30 sasa,hivyo baada ya kurusha sehemu ya tamthiliya ilichukuliwa hapa itaongeza soko la wageni kutoka nchi zinazozungumza kijerumani,kwa sababu wanajua tunafanya utafiti,tmekwisha fka hapa mara mbili na kukutana na mtaalamu na kutuonesha maeneo ,wanajua tunachukua maeneo mazuri,hoteli nzuri,tuna taarifa  na vifaa vya kutosha,hivyo kutakuwa na matokeo makubwa katika Utalii “alisema Lessnick.

Kuhusu Maudhui ya Tamthiliya hiyo ambayo inaoneshwa kwa zaidi ya miaka 30 sasa ,Mona Lessnick amesema imebeba maudhui ya aina tatu ambayo ni Vichekesho,Mahusiano pamoja na Drama.
 
“Ni Burudani kwa familia,tuna hadithi tatu,katika hadithi kuu watu wanasafiri kwa meli kuizunguka nchi,wakasafiri kuja Tanzania ,kuna hadithi nzuri za mahusiano ambazo vipande vyake vimechukuliwa Tanzania “alisema Lssnick.


“Katika muongozo tuna aina tatu ya hadithi,tuna hadithi ya mapenzi,tuna hadithi ya vichekesho na drama hii tunayofanya leo ni vichekesho,tuna watu wawili ,katika muongozo wa kwanza inaonesha watu haw wamepata tatizo katika gari lao hapa  Serengeti,lakini tulipaa ugumu kupiga picha ndio tukapata mahala hapa pazuri kwa kufanya video,tukafanya Drama hapa ya gari kukwama ndani ya maji na gari nyingine ikaja nyuma kuoka watu hawa wakiw wamekaa juu ya gari lao na kuondolewa katika maji”alisema Schroeder.

Tamthiliya ya Dream Boat imefikisha miaka 35 sasa tangu kuanza kurushwa katika vituo mbalimbali vya Televisheni nchini Ujerumani na kwamba sehemu mbili zenye urefu wa dakika 90 kila moja za tamthiliya hiyo ,picha zake hupigwa katika nchi moja ya kiafrika .

Mwisho.



No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages