Pages

VIJANA 150 WAKUTANA KAHAMA KWENYE BONANZA LA MICHEZO LILILOANDALIWA NA AGPAHI

Vijana wanaotoka katika halmashauri za wilaya ya Kahama Mji,Ushetu,Msalala na Manispaa ya Shinyanga wamekutana katika bonanza la michezo lililoandaliwa na Shirika la Kitanzania lisilo la kiserikali la Ariel Glaser Pediatric Aids Healthcare Initiative (AGPAHI) linalojihusisha na mapambano dhidi ya Virusi vya UKIMWI na UKIMWI.

Bonanza hilo la michezo limejumuisha vijana 150 wenye umri kati ya miaka 14-19 wanaotoka katika klabu za vijana zilizoundwa na zinasimamiwa na shirika la AGPAHI kwa kushirikiana na halmashauri za wilaya husika.

Akifungua bonanza hilo katika uwanja wa taifa mjini Kahama leo Jumamosi Desemba 17,2016,mgeni rasmi Dr. Anthony Kasomelo kutoka hospitali ya mji wa Kahama,alisema bonanza hilo ni kwa ajili ya vijana kufurahi,kufahamiana,kupata marafiki wapya,kuonyesha vipaji na kujifunza. 

"Vijana hawa wanatoka kwenye vikundi 12 vilivyopo katika halmashauri nne za mkoa wa shinyanga,ambazo ni Msalala,Kahama mji,Ushetu na manispaa ya Shinyanga", alisema Kasomelo.



Dr. Kasomelo alitumia fursa hiyo kulipongeza shirika la AGPAHI kwa kuendelea kuwa karibu na vijana huku akiwaasa vijana hao kuendelea kuwa wafuasi wazuri wa huduma za afya ili kuboresha afya zao ili waweze kutimiza ndoto zao.


Aidha alitoa wito kwa viongozi wa halmashauri za wilaya kuendelea kutoa ushirikiano kwa shirika la AGPAHI hasa katika kutekeleza majukumu ya kuwasaidia wananchi katika huduma za afya hususani kwa watu wanaopata tiba na matunzo ili huduma zipatikane katika ubora na ziwe rafiki kwa wananchi. 

Awali akizungumza katika bonanza hilo, Afisa mradi wa watoto kutoka Shirika la AGPAHI mkoa wa Shinyanga, Jane Kashumba alisema wafadhili wa bonanza hilo ni shirika la Uingereza linalofadhili huduma za kuboresha maisha ya watoto (Children's Investment Fund Foundation -CIFF).

Kashumba alibainisha kuwa shirika la AGPAHI limeanzisha klabu 12 za vijana zenye wastani wa vijana 20 - 70 walio katika rika balehe. 



"Lengo la vikundi hivi ni kuwakutanisha vijana kila mwezi ili waweze kujifunza pamoja masuala mbalimbali ikiwemo masuala ya msukumo rika kwa vijana,kushirikiana katika kutatua changamoto zao na njia za kujikinga na maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi vijana hao wameendelea kunufaika na elimu hiyo",alieleza Kashumba. 



Miongoni mwa michezo iliyochezwa na vijana hao ni pamoja mpira wa miguu,kuvuta Kamba,mbio za magunia,kukimbiza kuku ,kuimba nyimbo na kucheza muziki ambapo washindi waliibuka na zawadi mbalimbali. 


Bonanza hilo limehudhuriwa na wadhibiti wa Ukimwi kutoka halmashauri za wilaya,wasimamizi wa klabu za vijana,wafanyakazi wa shirika la AGPAHI na wadau mbalimbali wa michezo na mambo ya afya. 

Angalia matukio katika picha yaliyojiri uwanjani hapa chini
Afisa mradi wa watoto kutoka Shirika la AGPAHI mkoa wa Shinyanga, Jane Kashumba akizungumza wakati Bonanza la michezo katika uwanja wa taifa wa mjini Kahama
Mgeni rasmi Dr. Anthony Kasomelo kutoka hospitali ya mji wa Kahama akifungua bonanza hilo la vijana lililokutanisha vijana 150 ambapo mbali na kulipongeza shirika la AGPAHI alitumia fursa hiyo kuwaasa vijana hao kupenda shule
Katikati ni mgeni rasmi Dr. Anthony Kasomelo akizungumza wakati wa kufungua bonanza la michezo.Kushoto ni Mhudumu wa jamii pia Afisa tabibu kutoka kituo cha afya cha Kolandoto katika manispaa ya Shinyanga Maryciana Bruno ,aliyeinama kulia ni Mganga mfawidhi zahanati ya Segese Denis Ngatale
Mgeni rasmi Dr. Anthony Kasomelo akiteta jambo na Jane Kashumba 
Timu ya mpira wa miguu kutoka halmashauri ya manispaa ya Shinyanga wakijiandaa kuanza mchezo baina yao na timu kutoka halmashauri ya wilaya ya Ushetu,Msalala na Kahama Mji. 
Wachezaji wa timu ya mpira wa miguu kutoka manispaa ya Shinyanga wakiwa na walezi wao na maafisa kutoka AGPAHI 
Wachezaji wa timu ya mpira wa miguu kutoka halmashauri ya wilaya ya Ushetu,Msalala na Kahama Mji wakipiga picha kabla ya mchezo 
Wachezaji wa timu ya halmashauri ya wilaya ya Kahama Mji,Ushetu na Msalala wakiwa na walezi wao na maafisa kutoka AGPAHI 
Dawati la ufundi timu ya Kahama Mji,Ushetu na Msalala. 
Mchezo kati ya Kahama Mji,Ushetu na Msalala ukiendelea 
Mchezo unaendelea ambapo hadi kipenga cha mwisho kinapulizwa Kahama mji walikuwa wanaongoza kwa kuibamiza timu ya manispaa ya Shinyanga bao 4-1 
Mbio za magunia ukiendelea kati ya vijana wa kike kutoka manispaa ya Shinyanga(waliovaa nguo za bluu) na wasichana kutoka Kahama Mji,Ushetu na Msalala zikiendelea 
Mbio za magunia zikiendelea ambapo hadi mwisho wa mchezo mshindi wa kwanza alikuwa Esther Peter kutoka Ushetu (aliyevaa nguo nyeupe),wa pili Elizabeth Busheye kutoka manispaa ya Shinyanga(wa kwanza kulia) 
Mbio za magunia upande wa vijana wa kiume kutoka manispaa ya Shinyanga (waliovaa nguo za bluu) na wasichana kutoka Kahama Mji,Ushetu na Msalala zikachukua nafasi 
Mchezo unaendelea,ambapo hadi mwisho wa mchezo mshindi wa kwanza alikuwa Ali Seleman,wa pili Isack Kiwila 
Mchezo wa kufukuza kuku upande wa vijana wa kike ukiendelea
Vijana wakiendelea kukimbiza kuku
Helena Daudi kutoka manispaa ya Shinyanga akiwa amebeba kuku baada ya kufanikiwa kumkamata na kisha kuondoka naye kama zawadi ya ushindi
Vijana wa kiume nao walifukuza kuku
Kijana Peter Kulwa naye akaondoka na kuku baada ya kufanikiwa kumkamata
Mchezo wa kuvuta kamba nao ulikuwepo,picha ni kushoto ni vijana wa kike kutoka Kahama mji,Ushetu na Msalala wakijiandaa kushindana kuvuta kamba na vijana wa kike kutoka manispaa ya Shinyanga(kulia).Waliopo katikati ni Dr. Anthony Kasomelo kutoka hospitali ya mji wa Kahama na Afisa mradi wa watoto kutoka Shirika la AGPAHI mkoa wa Shinyanga, Jane Kashumba wakitoa maelekezo kwa vijana hao kabla ya mchezo huo wa kuvuta kamba
Vijana kutoka manispaa ya Shinyanga wakijiandaa kuvuta kamba
Katika mchezo huo wa kuvuta kamba vijana kutokaUshetu,Msalala na Kahama Mji waliibuka washindi
Vijana wa kiume kutoka Kahama Mji,Ushetu na Msalala wakijiandaa kushindana kuvuta kamba dhidi ya vijana kutoka manispaa ya Shinyanga
Vijana kutoka manispaa ya Shinyanga wakikazana kuvuta kamba ingawa hata hivyo walishindwa katika mchezo huo
Vijana kutoka manispaa ya Shinyanga wakiimba shairi
Walezi wa vijana na vijana wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea uwanjani
Vijana kutoka Kahama mji wakiimba 
Kulia ni Dr. Selemani Wambili kutoka Zahanati ya Kagongwa wilayani Kahama na mlezi wa vijana kituo cha Segese katika halmashauri ya Msalala wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea
Vijana wakiwa eneo la tukio 
Vijana kutoka manispaa ya Shinyanga wakicheza muziki
Vijana wakionesha kipaji cha kucheza
Kijana akiimba wimbo 
Vijana wakishindana kucheza muziki
Wajumbe wa kamati ya kutoa zawadi kwa washindi katika michezo iliyofanyika uwanjani wakijadili jambo kabla ya kuanza kugawa zawadi kwa washindi.Aliyekaa kushoto ni Dr. Selemani Wambili kutoka Zahanati ya Kagongwa,kulia kwake ni mhudumu wa jamii kutoka kituo cha Kolandoto Maryciana Bruno.Waliosimama wa kwanza ni kushoto ni mlezi wa watoto kituo cha Kambarage Glory Assey akifuatiwa na mlezi wa watoto kituo cha hospitali ya Kahama mji Flora Selutongwe.Kulia ni mgeni rasmi Dr. Anthony Kasomela akijiaandaa kupokea majina ya washindi ili awape zawadi
Mgeni rasmi Dr. Anthony Kasomelo akitoa zawadi ya kombe kwa Timu ya Kahama mji,Ushetu na Msalala walioibuka washindi baada ya kuifunga timu ya manispaa ya Shinyanga bao 4-1
Vijana wakifurahia baada ya kupewa zawadi ya kombe
Vijana waliofunga magoli manne na kuipa ushindi timu ya Kahama mji,Ushetu na Msalala wakipokea zawadi ya saa kila mmoja
Vijana kutoka manispaa ya Shinyanga wakipokea zawadi kombe kwa kuibuka wachezaji bora wa muziki
Mgeni rasmi Dr. Anthony Kasomelo akimkabidhi zawadi ya saa Esther Peter kutoka Ushetu aliyekuwa mshindi wa kwanza katika shindano la mbio za magunia
Mshindi wa pili mbio za magunia upande wa vijana wa kike Elizabeth Busheye kutoka manispaa ya Shinyanga akipokea zawadi ya saa
Mshindi wa kwanza mbio za magunia upande wa vijana wa kiume Ali Seleman kutoka manispaa ya Shinyanga akipokea zawadi ya saa
Mshindi wa pili mbio za magunia Isack Kiwila kutoka manispaa ya Shinyanga akishikana mkono na mgeni rasmi kabla ya kupokea zawadi ya saa
Kijana aliyeonesha kipaji cha kucheza muziki akipokea zawadi ya begi
Mlezi wa vijana katika kituo cha hospitali ya mkoa wa Shinyanga Elizabeth Lubasha akijiandaa kupokea vifaa vya shule ikiwepo soksi na kalamu kwa ajili ya vijana anaowalea
Mlezi wa vijana katika kituo cha Segese Kanzaga Fabian akipokea vifaa vya shule kwa ajili ya vijana wake
Mlezi wa watoto kituo cha hospitali ya Kahama mji Flora Selutongwe akiwa amebeba zawadi ya soksi na kalamu kwa ajili ya vijana anaowalea

Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)