Pages

TIMU YA KIJITONYAMA VETERANS WAFANYA MKUTANO WA KUPATA VIONGOZI WAPYA

 TIMU ya Kijitinyama Veterans yenye maskani yake Kijitonyama, leo imefanya uchaguzi mkuu na kupata viongozi wapya wa kuingoza timu hiyo kwa kipindi cha miaka mitano.

Nafasi zilizokuwa zikigombewa ni tisa, ambapo katika nafasi ya Mwenyekiti aliyekuwa akishikilia nafasi hiyo muda uliopita, Lupyana Michael, ameendelea kubaki katika nafasi hiyo baada ya kupigiwa kura na wajumbe na kuongoza dhidi ya mpinzani wake, Petro Malima .

Pia aliyekuwa Katibu Mkuu wa Timu hiyo Amon Petro, naye ameendelea kubaki katika nafasi hiyo baada ya kuibuka na kura nyingi zaidi ya mpinzani wake, Evodius Mtawala

Naye Mratibu wa timu hiyo, Majuto Omary,pia ameendelea kubaki katika nafasi hiyo baada ya kuibuka kidedea dhidi ya mpinzani wake Evans Malla, 

Kwa mujibu ya utaratibu wa Timu hiyo, kutokana na mapendekezo ya Wajumbe, katika uchaguzi, majina mawili yanayopigiwa kura na mmoja kati yao anayepata kura nyingi ndiye anapaswa kuwa kuwa kiongozi katika nafasi husika na anayefuatia kwa kura anakuwa msaidizi.

VIONGOZI WALIOCHAGULIWA:-

MWENYEKITI:  Lupyana Michael
MAKAMU MWENYEKITI: Malima Petro

KATIBU MKUU: Amon Petro
KATIBU MSAIDIZI: Evodius Mtawala

MRATIBU MKUU: Majuto Omary
MTARIBU MSAIDIZI: Evans Malla

MWEKAHAZINA MKUU: Othaman Hussein 
MWEKA HAZINA MSAIDIZI: Sweetbert Mwombeki

MSEMAJI WA TIMU: Muhidin Sufiani (Mafoto)


 Baadhi ya wajumbe wakipitia vifungu vya katiba wakati wa uchaguzi huo.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)