- Mwasilisha mada (wa pili kulia) akijadiliana jambo na baadhi ya watendaji na wataalamu kutoka sekta za Maji, Afya na Elimu pamoja na wale wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wakati wa warsha hiyo iliyoandaliwa na TGNP Mtandao.
- Sehemu ya watendaji na wataalamu kutoka sekta za Maji, Afya na Elimu pamoja na wale wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wakijadiliana jambo katika warsha iliyoandaliwa na TGNP Mtandao.

- Meneja Idara ya Ujenzi wa Nguvu za Pamoja, TAPO kutoka TGNP Mtandao, Grace Kisetu (kushoto) akizungumza na washiriki wa warsha hiyo.
- Mwasilisha mada akizungumza na washiriki wa warsha hiyo.
- Watendaji na wataalamu kutoka sekta za Maji, Afya na Elimu pamoja na wale wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya majadiliano.
MTANDAO wa
Jinsia Tanzania (TGNP) inakutanisha watendaji mbalimbali na wataalamu
kutoka sekta za Maji, Afya na Elimu pamoja na wale wa Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kuangalia changamoto za
kijinsia zilizopo kwenye sera za sekta tajwa.
Watendaji
hao na wataalamu wanaoungana na wengine kutoka Halmashauri zote za jiji
la Dar es Salaam pamoja na wanajamii kuangalia changamoto za kijinsia
lengo likiwa ni kuboresha zaidi huduma ndani ya sekta hizo.
Akizungumza
katika warsha iliyowakutanisha wataalamu hao Meneja Idara ya Ujenzi wa
Nguvu za Pamoja, TAPO kutoka TGNP Mtandao, Grace Kisetu alisema lengo
kubwa la majadiliano hayo ni kushauriana namna bora ya utekelezaji wa
sera katika sekta hizo zinazotegemewa zaidi na jamii.
Wataalamu
hao watatoka na kikosi kazi cha wataalamu ambacho pamoja na mambo
mengine kitaweka mikakati ya pamoja ili kufuatilia kwa karibu
utekelezaji wa sera kwa wadau anuai.

No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)