TBL yatunukiwa tuzo ya kimataifa ya Mwajiri bora nchini - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

TBL yatunukiwa tuzo ya kimataifa ya Mwajiri bora nchini

 
Taasisi ya kimataifa ya masuala ya Raslimali Watu na ajira ijulikanayo kama Top Employer Institute yenye Makao yake makuu nchini Uholanzi imeitunukia tuzo ya Mwajiri Bora 2017 nchini Tanzania kampuni ya Bia Tanzania kutokana na kuzingatia na kutekeleza kanuni za Raslimali Watu na uajiri ipasavyo.
 
Tuzo hii ilikabidhiwa  katika hafla iliyofanyika  katika kiwanda cha Ilala jijini Far es Salaam na kuhudhuriwa na menejimenti na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni.TBL ilitangazwa rasmi kuwa mshindi wa tuzo hii katika hafla iliyofanyika Johanesburg nchini Afrika  mapema mwezi Oktoba mwaka huu.
 
Vigezo vya ushindi vimetokana na utafiti wa taasisi ya Top Employers kwa makampuni mbalimbali makubwa nchini ambao ulilenga kwenye  utekelezaji kanuni za ajira na Raslimali watu ambapo kampuni ya TBL imebainika kuwa na vigezo vya  ubora katika utekelezaji wa kanuni za ajira zinazotakiwa na kutangazwa kuwa  kampuni bora  inayoongoza katika masuala ya ajira kwa kipindi cha mwaka ujao wa 2017.
 
Baadhi ya vigezo ambavyo vilifuatiliwa katika utafiti huo kutoka kwa waajiri ni mikakati ya kukuza vipaji vya wafanyakazi,mpangilio wa kazi wa kila siku,mazingira ya kazi,uendelezaji wafanyakazi kimafunzo,utawala sehemu za kazi,taaluma na upandishaji wa vyeo kwa wafanyakazi,maslahi ya wafanyakazi na malipo ya stahiki zao kwa ujumla na desturi ya kampuni.
 
 
Akiongea wakati wa hafla hiyo Mkuu wa taasisi ya Top Employer Institute kanda ya Afrika, Billy Elliot , amesema suala kubwa ambalo limeangaliwa ni kwa jinsi wafanyakazi wanavyopata fursa ya kujiendeleza kibinafsi na kukuza taaluma zao “Baada ya kufanya thamini ya vigezo vyote hivi tumebaini kampuni ya Tanzania Breweries Limited inakidhi kiwango cha kuwa mwajiri bora nchini Tanzania”.Alisema Billy Elliot.
 
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Raslimali Watu wa TBL, David Magese  alisema “Hatua hii ya kampuni yetu kutangazwa kuwa Mwajiri bora na taasisi ya kimataifa ya Top Employers Institute ni uthibitisho kuwa tumekuwa tukitekeleza kanuni bora za Raslimali watu na uajiri ambayo msingi wake mkubwa ni kujali maslahi ya wafanyakazi na kuboresha mazingira ya kazi”.Alisema.
 
Magese aliongeza kusema kuwa TBL mbali na kushinda tuzo hii ya uajiri bora ngazi ya kimataifa pia inashikilia rekodi ya kuwa mwajiri bora nchini ambapo mwaka 2015 ilishinda tuzo ya Mwajiri Bora inayotolewa na Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE). “Tunajivunia kwa mafanikio ya kampuni inayoendelea kuyapata na tutazidi kuboresha mazingira ya kazi kwa wafanyakazi wetu kwa kuwa ni moja ya sera yetu”.Alisema Magese.
 Wafanyakazi wa TBL  kitengo cha Rasimali watu wakiwa katika picha ya pamoja  wakati wa hafla hiyo.
 Wafanyakazi wa TBL Group wakimsikiliza kwa makini Meneja wa kanda ya afrika wa taasisi ya Top Employers Instututes, Billy Elliott   wakati wa hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Mkurugenzi wa Rasilimali watu wa TBL Group ,David Magese akikabidhiwa  tuzo ya Top Employer Tanzania 2017 na  Top Employers Istitute ,Region Manager Africa  Billy Elliott  wakati wa hafla iliyofanyika Ilala jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages