TBL Group yawaasa madereva kuwa makini msimu huu wa sikukuu - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

TBL Group yawaasa madereva kuwa makini msimu huu wa sikukuu

Katika mkakati wake wa kuunga mkono jitihada za serikali za kupunguza ajali za barabarani nchini,kampuni ya TBL Group imedhamini mafunzo ya Usalama Barabarani kwa waendesha Bajaji na pikipiki wanaofanyia kazi zao katika kituo cha Ubungo Maji .
Madereva pia walipata fursa ya kupata mafunzo ya Unywaji wa Kistaarabu ambayo yanaelekeza kutumia vinywaji vyenye kilevi kistaarabu na kuhakikisha utumiaji wake hauleti athari yoyote ambapo pia madereva walikumbushwa kutoendesha vyombo vya moto wakiwa wametumia vinywaji vyenye kilevi.

Meneja wa Masuala Endelevu wa TBL Group,Irene Mutiganzi ,alisema kampuni imedhamini  mafunzo hayo yaliyotolewa na Maofisa kutoka  Jeshi la Polisi,Kitengo cha Usalama Barabarani ni mwendelezo wa kampuni hiyo kuendesha kampeni za usalama barabarani.

Tukiwa kampuni inayotengeneza vinywaji vya aina mbalimbali vyenye kilevi tunalo jukumu pia kuunga mkono jitihada za serikali kupunguza matukio ya ajali za barabarani ambazo zimekuwa zikisababisha vifo vya watu wengi na hasara kubwa.Hivyo tunatoa wito kwa madereva wote hususani wa vyombo vya moto katika msimu huu wa sikukuu kuwa makini kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kuepusha ajali zinazotokana na uzembe wa kutozingatia sheria na kanuni za usalama barabarani”.Alisema Mutiganzi.

Mutiganzi alisema TBL Group itaendelea kuunga mkono jitihada za serikali na wadau wengine wa masuala ya usalama barabarani ili  kutokomeza matukio ya ajali nchini.

Alisema hivi sasa kampuni inaendesha mafunzo ya unywaji wa kistaarabu kwa makundi mbalimbali ya kijamii ikiwemo madereva na elimu hiyo itaendelea kutolewa kwa nguvu zote katika kipindi cha mwaka ujao ili iwafikie watanzania wengi nakubadilisha jamii kuwa na utamaduni wa utumiaji wa vinywaji vyenye kilevi bila kusababisha athari zozote kutokana na utumiaji huo.


“kampuni pia imekuja na mkakati wa kuhakikisha elimu ya usalama barabarani inawafikia wanafunzi wa shule za msingi ili wakue wakiwa na uelewa wa umuhimu wa kuzingatia kanuni za usalama barabarani ambapo kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani imeanza kuendesha imekuwa  mafunzo kwa wanafunzi wa shule za msingi katika mikoa  mbalimbali nchini"alisema
Madereva wa bajaj na Pikipiki (bodaboda) wakimsikiliza kwa makini mrakibu Msaidizi wa Polisi Kitengo cha Elimu  Makao Makuu ya Kikiosi cha Usalama Barabarani nchini,ASP Mossi Ndozero (Kulia)  wakati  wa   mafunzo  ya usalama barabarani kwa madereva wa bajaji na pikipiki (bodaboda) yaliyofanyika eneo la Ubungo maji  jijini Dar es Salaam chini ya udhamini wa kampuni ya TBL Group ili kuwafanya madereva hao waweze kuendesha kwa usalama katika msimu huu wa sikukuu za mwisho wa mwaka
Wafanyakazi wa TBL Group  kitengo cha Uhusiano, Irene Mutiganzi  (kushoto ) na Amanda Walter wakimsikiliza kwa makini  Mrakibu Msaidizi wa Polisi Kitengo cha Elimu  Makao Makuu ya Kikiosi cha Usalama Barabarani nchini,ASP  Mossi Ndozero (Kulia)   wakati   wa  mafunzo ya elimu ya usalama barabarani kwa madereva wa bajaj na pikipiki (bodaboda) eneo la Ubungo maji  jijini Dar es Salaam yaliyofanyika kwa udhamini wa TBL Group.

Madereva wa Bajaj na pikipiki maarufu kwa jina laBodaboda wanaofanya kazi katika sehemu ya  Ubungo Maji jijini Dar es Salaam, wakimsikiliza kwa makini Mwalimu wa mafunzo ya usalama barabarani Jeshi la Polisi  kutoka   Makao Makuu ya Kikosi cha Usalama Barabarani S/SGT  Dina Mosi wakati alipokuwa akiendesha mafunzo ya Usalama barabarani .Mafunzo hayo yalifanyika kwa udhamini wa kampuni ya  TBL Group.
Mwalimu wa Mafunzo ya usalama wa barabarani wa jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani ,S/SGT Dina Mosi,(kulia) akimfafanulia jambo mmoja wa madereva  wa  bodaboda Juma Hamisi , wakati wa mafunzo hayo.
Abiria Khalfan Idd akisaidiwa kuvishwa kofia ngumu na  Mwalimu wa Mafunzo ya usalama wa barabarani wa jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani ,S/SGT Dina Mosi wakati alipokuwa akitoa elimu ya mafunzo kwa vitendo kwa madreva wa bodaboda  eneo la Ubungo Maji jijini Dar es Salaam,mafunzo hayo yalidhaminiwa na kampuni ya TBL Group

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages