Proinbox kukufurahisha wewe na familia yako Msimu huu wa sikukuu. - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Proinbox kukufurahisha wewe na familia yako Msimu huu wa sikukuu.

 
Zikiwa zimebaki Siku tano kukaribia sikukuu ya Noel almaarufu kama Christmass na Mwaka mpya, Christmass na mwaka mpya ni moja ya sikukuu kubwa sana duniani ambayo husherehekewa sana na watu mbalimbali duniani Kote. 

Sikukuu hii ya Christmass husherehekewa sana na wakristu ambapo wakristu hukumbuka siku ya Kuzaliwa kwa Yesu, na sikukuu hii huwafanya watu mbalimbali hupenda kushinda na familia zao pamoja huku wakifurahia kuadhimishwa kwa kuzaliwa kwake.

Katika Kipindi hiki cha sikukuu ya Christmass na mwaka mpya inapendeza unapokuwa nyumbani kwako ukifurahia pamoja na familia yako, moja kati ya burudani ambayo unaweza kufurahia na familia yako nikutazama filamu za nyumbani yaani filamu za kitanzania zenye ubora wa hali ya juu kabisa.

Filamu hizi hupelekea familia kufurahia na kujifunza mambo mbalimbali ambapo katika kipindi hiki cha sikukuu ya Christmass na Mwaka mpya basi utafurahia filamu nyingi na mpya kila siku kupitia Application yako ya ProinBox.

ProinBox ni moja kati ya application inayokuwezesha wewe mtazamaji kufurahia kutazama sinema za kitanzania zenye ubora wa hali ya juu kabisa kupitia simu yako ya mkononi huku ukizipata kwa bei nafuu kabisa.

ProinBox inakuwezesha kutazama moja kwa moja kupitia simu yako ya mkononi au kuipakua kwenye simu na kuweza kuitazama kwa bei nafuu kabisa, ProinBox inakupa nafasi ya kukurahisishia upatikanaji wa sinema za kitanzania kiganjani mwako ambapo unaweza pia kutazama filamu hizo kupitia tv yako kwa wale wenye Runinga zinazoruhusu teknolojia ya internet.
Soko la filamu Tanzania limeanza kukua kwa kasi huku Kampuni ya Proin promotions kutumia vizuri teknolojia katika kuhakikisha filamu za kitanzania na zenye ubora wa hali wa juu zinawafikia wadau wote na kwa muda mfupi huku ikiokoa muda wa wapenzi wa filamu kwenda kwenye maduka ya sinema kutafuta sinema hizo na muda mwingine bila mafanikio.

Proinbox inakurahisishia maisha wewe mtazamaji na mpenzi wa sinema za kitanzania kutopoteza kwenda kutafuta sinema hizo madukani ilhali sinema hizo hizo unauwezo wa kuzipata kupitia simu yako na kwa bei nafuu kabisa huku ukiokoa muda na gharama nyingine zinazokwepeka.

Furahia msimu huu wa sikukuu za Christmass na Mwaka na proinbox huku ukifurahia ubora wa filamu za kitanzania 

Unaweza kuipata application hii kupitia google playstore kwa wale wanaotumia simu au vifaa vinavyotumia mfumo wa android na pia kwa wale wanaotumia mfumo wa IOS pia wanaweza kuipata application hii kupitia App Store na kuihifadhi kwenye simu yako kisha kujiunga na kuanza kufurahia msimu huu wa sikukuu kwa kupata filamu mpya na zenye ubora wa hali ya juu sana.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages