Pages

Njia 6 Sahihi za Kuosha Gari lako.

Kuosha magari sio kazi ya kila mtu bali ni kazi ya watu wenye uelewa na uweledi wa kazi hiyo huku ukiifurahia kazi hiyo. 

Bahati mbaya sana watu wengi wamekuwa hawatumii vifaa sahihi katika uoshaji wa magari yao na hata wale wanaomiliki sehemu za kuoshea magari baadhi yao nao wamekuwa hawana vifaa sahihi katika kuosha magari ya wateja wao na badala yake wao hufikiria kuwa na sabuni, maji na mashine ya kutolea maji kwa spidi ndio kuweza kuosha gari huku wakidhani wanapatia kumbe ndio wanaharibu magari yao au hata ya wateja wao. Leo tutaangalia Njia sahihi tano za kuosha magari yetu.

1:Usitumie Maji ya Chumvi katika Kuosha Gari lako:

Wenye magari wengi wamekuwa na tabia ya kutopenda kufahamu maji yanayotumika kuoshea magari yao kama ni ya chumvi au laah.Usitumie Maji ya Chumvi katika kuosha gari lako kwasababu maji ya chumvi hupelekea kwanza kuondoa rangi ya gari lako taratibu lakini pia maji ya chumvi hupelekea kusababisha gari lako kushika kutu lakini pia Vioo vya gari lako kuwa na vidotidoti. Usipende kutumia maji ya chumvi katika kuosha gari lako.
2: Usitumie Sabuni ambazo sio sahihi kwaajili ya Kuoshea Magari:
Madereva wengi wanadhani sabuni ni sabuni tu na hazina tofauti, Hapana Sabuni zinatofautiana sana na pia kila sabuni imetengenezwa kwa matumi yake tu mfano sabuni iliyotengenezwa kwaajili ya kusafisha chooni huwezi kuitumia kusafishia vyombo kwanini?kwasababu madawa malighafi iliyotumika kutengeneza sabuni hio ilikusudiwa kwaajili ya chooni na vifaa vyote.

Kutumia sabuni ambayo sio sahihi katika kuoshea gari basi fahamu kuwa unapelekea kuharibu gari lako katika rangi ambapo kutumia sabuni ambayo sio sahihi kabisa hupelekea hatua ya kusababisha kutu kwenye gari kutokana na kuwa sabuni isiyo sahihi hupelekea kuondoa rangi ya gari lako na kuruhusu kutu kuinyemelea huku ikipelekea uvutaji wa gari hilo baada ya kuonsha kuwa mgumu kwenye kulifuta. Usitumie Sabuni ya kuoshea vyombo wala sabuni ya Kufulia (Unga) katika kuoshea gari lako badala yake tafuta sabuni sahihi kwaajili ya kuoshea magari. Na sababu hizi zinapatikana katika maduka mbalimbali ya vifaa vya magari.

3:Osha gari lako likiwa Kivulini:
Ni muhimu sana kuosha magari yetu kwenye sehemu iliyotengenezwa kuzuia miale ya jua. Kwanini ni muhimu kufanya hivyo kwasababu unapoosha gari lako kwenye jua hupelekea kukaushwa  kwa maji na sabuni kitu ambacho hupelekea gari kuwa na michilizi ambayo inakuwa migumu kutoka wakati wa kufuta gari mara baada ya kuosha 

4:Osha gari lako Kuanzia Juu kushuka Chini:
Unapoosha gari lako anza kuosha gari kuanzia Juu kwenye roof ukishuka chini, Unaweza kuanza kwenye roof ukafuatia kwenye Vioo na ukashuka mpaka kwenye milango, boneti na mwisho ukaosha matairi na rim zake. Kufanya hivi hupelekea uchafu unaotoka juu kutiririka chini na gari lako kusafishika vizuri.

5:Safisha Matairi na rim zake:
Moja ya kitu kinachopelekea gari lako kuonekana vizuri ni matairi na rim kuwa safi ambapo sawa na bodi ya gari lako pia linapokuwa safi uongeza mvuto na kupendezesha zaidi. Pia katika kusafisha matairi na rim unashauriwa kutumia vifaa sahihi kwaajili ya kutotumia sabuni yoyote yenye acid ambapo ukitumia sabuni yenye acid hupelekea kusabababisha kutu kwenye drum za tairi na rim pia huku ikiondoa rangi kwenye rims

6:Safisha Gari lako ndani:
Kusafisha ndani ya gari huchukua dakika 10 hadi 15 wakati wa kusafisha gari lako ndani unapaswa kuondoa na kutupa vitu vyote vilivyomo ndani ya gari ambavyo havina kazi na wala havitumiki tena hii itakusadia gari lako kuonekana nadhifu na lenye mvuto ndani.

Tumia vifutio laini katika kufuta sehemu kama dashboard, milango, ndani ya mifuko ya milango, katikati ya gari kwenye viti na sehemu nyingine kwaajili ya kuondoa vumbi na uchafu.

Lakini pia unashauriwa kupulizia Air fresh kwenye sehemu za kutolea AC ili kufanya gari lako kuwa na harufu ya kuvutia pindi uwashapo kiyoyozi ndani ya gari. Na pia nyunyizia spray ya kusafishia vioo kwenye kipande cha karatasi na safisha vioo vyako taratibu kwa kufanya hivyo hupelekea kuondoa baadhi ya madoa doa kwenye vioo na kufanya vioo vyako kuwa visafi na vinavyong'aa zaidi.

Usafishapo ndani ya gari lako hakikisha unatumia mashine ya kuvutia uchafu ijulikanayo kama Vacuum, mashine huvuta vumbi na uchafu ambao ni vigumu wewe kufikisha mkono wako kusafisha na pia kuondoa hata uchafu ambao hauzoleki kwa mikono. Hii itakusaidia kulifanya gari lako kuwa safi ndani na lenye kuvutia lakini kabla ya hapo unatakiwa kuondoa makapeti ya gari lako na kuyasafishia nje kwa kutumia mashine kwa yale makapeti ya vitambaa na kwa makapeti ya plastiki au mpira unatakiwa kusafisha kwa maji na kuyaanika yakauke lakini pia unaweza kuyafua makapeti yako ya kitambaa na kuyaanika juani kama una muda wa kutosha kuyasubiria kukauka.

Baada ya kumaliza hayo yote rudisha kila kitu sehemu yake na fungua milango yote na kupulizia air fresh vizuri na kuiacha isambae ndani taratibu.

Baada ya hapo unaweza kuendelea na Safari yako huku gari likiwa safi na lenye mvuto


Je unahitaji kununua gari Kutoka Japani?Basi usisite kuwasiliana na Mimi kwa Namba  0712 390 200 na nitakupatia gari uipendayo kwa Bei Nzuri tu na offer kibao ndani ya msimu huu wa XMass na Mwaka Mpya.

9 comments:

  1. Thanx bro for the Tips

    ReplyDelete
  2. Samahani ndugu nina swali, je nisabuni gani inatumika kuoshea gari,, na inaitwaje

    ReplyDelete
    Replies
    1. Sabuni zipo nyingi sana na majina ni mengi. Kikubwa nenda kwenye maduka yanayouza vifaa vya urembo wa magari na ulizia sabuni maalumu ya kuoshea magari na watakuonyesha

      Delete
  3. Nafikiria kufungua car wash ya kima can chini lakini sina uzoefu wa kutosha kwenye mahari hata uoshaji wa injini na chassis,nipo tayari kujifunza kama utanikaribisha Kaka,Asante kwa elimu hii

    ReplyDelete
    Replies
    1. Karibu mkuu tubadilishane mawazo katika hili na tuendelee kujifunza

      Delete
  4. Hongera kwa Elimu nzuri nakuja inbox

    ReplyDelete

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)