Pages

Makomandoo wa JWTZ kivutio sherehe za Uhuru Jana

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, Desemba 9, 2016 amewaongoza mamilioni ya watanzania kusherehekea Uhuru wa Tanzania Bara kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, ambapo kivutio kikubwa kilikuwa kikosi maalum cha Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania, Makomandoo ambapo pamoja na kuonyesha umahiri wao katika medani za kivita, lakini kubwa ni komandoo hao kulala juu ya misumari yenya ncha huku wengine wakimkanyaga mwenzao aliyelalia misumari, kifuani. Pichani Komandoo huyo akionyesha maajabu hayo. (PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
 Komandoo wakionyesha jinsi ya kupambana na adui bila ya kutumia silaha
 Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Rais John Magufuli, akikagua gwaride wakati wa maadhimisho hayo.  
 Rais aksialimiana na Waziri Mkuu, Mh. Kassim Majaliwa
 Makamu wa Rais, Bibi Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa
 
 Baadhi ya wananchi wakitazama kutokea uwanja waTaifa kilichokuwa kikiendelea kwenye uwanja wa Uhuru
 Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa, akizungumza jambo na Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohammed Shein
Amiri Jeshi waMjeshi ya Ulinzi na Usalama, Rais John Magufuli, akiwa na Mkuu wa Majeshi, Jenerali Davis Mwamunyange, akiwapungia wananchi wakati akiwasili kwenye uwanja wa Uhuru akiwa kwenye gari la wazi la Kijeshi
 
 
 

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)