MWANAFUNZI WA KIDATO CHA TATU ANUSURIKA KUFA MARA BAADA YA KUBWAKWA NA KUTELEKEZWA KORONGONI - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MWANAFUNZI WA KIDATO CHA TATU ANUSURIKA KUFA MARA BAADA YA KUBWAKWA NA KUTELEKEZWA KORONGONI

Image result for KAMANDA WA POLISI
 ARUSHA MKUMBO
Kamanda wa Polisi Mkoani Arusha Charles Mkumbo
 
 Na Woinde Shizza,Meru

MWANAFUNZI wa kidato cha tatu katika shule ya sekondari Kitefu iliyopo Meru  mkoani Arusha amenusurika kufa mara baada ya kubakwa na
kuteketezwa kwenye  korongo la mchanga na kusababishiwa  maumivu makali yaliyomsababishia kushindwa kuendelea na masomo yake kwa muda.

Akielezea tukio hilo  mwanafunzi huyo ambae amehifadhiwa jina kwa sababu za kimaadili alisema kuwa tukio hilo lilitokea novembar 13 majira ya saa
12.30 alipotoka kwa kinyozi.

Alisema kuwa ghafla akiwa anarudi nyumbani alikutana na mtu huyo
aliyemfanyia kitendo hicho na kuanza kumkaba shingoni na kumziba mkono ili asitoe sauti na ndipo alipomfanyia kitendo hicho cha ukatili
ambacho kimemfanyia ashindwe kuendelea na masomo yake vizuri.

"Nilijitahidi sana kupiga kelele ila kutokana na alivyokuwa amenikaba shingoni alinifanyia kitendo hiki kikatili ambacho kimejipelekea nishindwe
kuendelea na masomo yangu kwani baada ya vipimo nimeonekana aliniumiza sehemu nyingi ikiwemo hata kifua changu"alisema mwanafunzi huyo.

Kwa upande wake mama mzazi wa mwanafunzi huyo aliyejitambulisha Rambikiaeli Akyoo alisema kuwa kutokana na vitendo vya ukatili kukithiri kwa mabinti zao ni vema serikali ikawa inawachukulia hatua mapema wanaohusika kwani tangu akamatwe mtuhumiw huyo na kupellekwa kituoni bado hajasomewa shtaka linalomkabili hivyo kufanya wanaohusika na
vitendo hivyo kuona wako sawa kwa vile hakuna hatua kali inayochukuliwa mapema dhidi ya matukio hayo

Nae mkuu wa shule hiyo Nkoe Nicolaus  alisema kuwa tukio hilo limemfanya
mwanafunzi huyo aathirike kisaikolojia kwani tangu afanyiwe ukatili
huo ameshindwa kiendelea na masomo yake vizuri hivyo anawashauri
wazazi wa binti huyo kumuhamisha shule hiyo na kumuhamishia
nyingine ili kimbadilisha mawazo ya kifkra.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kitongoji cha kitefu tanesco Samweli
Matayo alikiri kutokea kwa tukio hilo katika kitongoji chake na kusema kuwa mara baada ya taarifa walifanikiwa kumtia hatiani mtuhumiwa aliyetambulika kwa jina la Wilson  Elias ambae ndie  aliyehusika na ukatili huo  na kumfikisha katika kituo kidogo cha polisi usa river ili kukabiliana na shutuma hizo.

Kamanda wa  polisi  Charles Mkumbo amethibitisha kukamatwa kwa
mtuhumiwa huyo ambapo limesema kuwa mtuhumiwa alikamatwa kwa rb namba RB/R/4250/2016  na atafikishwa mahamani upelelezi ukikamilika.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages