Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee naWatoto Dk. Mpoki Ulisubisya (kulia), akizungumza na viongozi mbalimbali wa sekta ya afya wakati akizindua mpango wa huduma maalumu kwa wateja wakubwa Dar es Salaam leo asubuhi.
Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Profesa Mohamed Janabi (kushoto), akizungumza katika hafla hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu akizungumza kwenye mkutano huo.
Meneja Huduma kwa Wateja wa MSD, Salome Malamia akizungumza katika hafla hiyo.
Mmoja wa maofisa kutoka Ofisi ya Inayosimamia Utekelezaji wa Mapendekezo ya Maboresho (SMO), Naomi Shangani akitoa maelezo kwa mgeni rasmi kuhusu mpango huo.
Ofisa wa SMO, Frankie Nkone akieleza kazi za eneo lake zinavyofanyika.
Kikosi kazi cha SMO. kutoka kushoto ni Benjamin Mtesigwa, Frankie Nkone, Naomi Shangali, Marko Masala na kiongozi wao, Cosmas Nalimi. |
Naomi Shangali (kulia), akiwaelekeza jambo wenzake.
Wajumbe wa mkutano huo kutoka sekta ya afya wakiwa wameinamisha vichwa vyao kwa dakika moja kumkumbuka aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya MSD, marehemu Profesa Idrissa Mtulia aliyefariki jana.
viongozi wa sekta ya afya wakiwa kwenye hafla hiyo.
mazungumzo ya hapa na pale yakiendelea.
Mgeni rasmi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee naWatoto Dk. Mpoki Ulisubisya (kulia), akiwa na viongozi wenzake katika uzinduzi huo.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Baadhi ya wafanyakazi wa MSD wakiwa kwenye hafla hiyo.
Viongozi wa sekta ya afya wakiwa wameinua mikono juu kuridhia mpango wa huduma maalumu kwa wateja wakubwa wakati wa uzinduzi wa mpango huo ulioandaliwa na Bohari ya Dawa (MSD), katika hafla iliyofanyika Dar es Salaam leo.
Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na maofisa wa SMO.
Picha ya pamoja ya viongozi na mgeni rsami.
Na Dotto Mwaibale
BOHARI ya dawa (MSD) imezindua mpango wa huduma maalumu kwa wateja wake wakubwa, kama moja ya hatua za kuboresha huduma kwa wateja.
Mpango huo utawawezesha wateja hao kupata huduma ya haraka zaidi pindi wanapokuwa wanahitaji mahitaji yao.
Wateja hao ni pamoja na hosipitali ya Taifa ya Muhimbili, Taasisi ya Mifupa (MOI), Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, hosipitali ya Sekoutoure Mwanza, Hosipitali ya Kibong’oto, Mirembe, Hosipitaliza Amana, Temeke, Mwananyamala, KCMC, Hospitaliya Benjamin Mkapa na Taasisi ya Moyo ya JakayaKikwete.
Akizindua mpango huo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee naWatoto Dk. Mpoki Ulisubisya amesema mpango huo ni moja ya maboresho yanayofanywa na MSD, ili kuhakikisha huduma zake zinatolewa kama inavyohitajika.
Dk. Mpoki pia amewasisitiza wateja hao wakubwa wa MSD kuhakikisha wanafanya maoteo sahihi ya mahitaji yao na kuyaleta MSD kwa wakati ilikuepusha ucheleweshwaji wa taratibu za manunuzi ambao pia tasababisha dosari kwenye upatikanaji wa dawa kwa wateja.
Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu amesema hatua ya kuwahudumia wateja hao kwa kiwango kizuri na cha uhakika itafanikiwa, hivyo Watarajie maboresho makubwa ya huduma.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)