MAAMUZI YA RUFAA YA KESI YA LEMA KUJULIKANA JANUARI 4, 2017 - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MAAMUZI YA RUFAA YA KESI YA LEMA KUJULIKANA JANUARI 4, 2017

Na.Vero Ignatus Arusha.

Mahakama kuu kanda ya Arusha imesikiliza maombi ya rufaa yaliyowasilishwa na  upande wa jamhuri na ule wa mshtakiwa Godbless Lema ambapo pande zote mbili wamekubaliana kusikilizwa rufaa ya upande wa jamhuri ambapo upande wa serikali wameiomba mahakama kuwasilisha kwa hati ya maandishi hapo kesho tarehe 30 disemba 2016


Aidha rufaa hizo ni pamoja na ile ya upande wa Jamhuri kutoridhika na maauzi ya Jaji Dkt. Modesta Opiyo la kuwapa siku kumi (10) upande wa mshtakiwa Lema kufaili notisi ya rufaa ,na upande wa wamshtakiwa ni ile ya kupinga uamuzi wa mahakama ya chini kushindwa kumpa lema masharti ya dhamana


Jaji aliyekuwa anasikiliza kesi ya rufaa hizo Salma Magimbi amesema kuwa mara baada ya upande wa jamhuri kuleta rufaa kwa njia ya maandishi upande wa mshtakiwa Lema wataijibu tarehe 30 disemba 2016 ambapo tarehe 2 januari watakutana pande zote kwaajili ya kufanya majumuisho

na maamuzi ya rufaa hiyo yatatolewa tarehe 4 januari 2017


Hata hivyo baada ya kusikiliza rufaa hizo mahakama imeibua hoja yenyewe na kuwapa kazi mawakili wa pande zote mbili kuangalia kuwa notisi iliyowasilishwa na mahakama ya chini imekidhi matakwa ya kisheria?


Kwa upande wa wakili wa mshtakiwa Peter Kibatala amesema kuwa kwa upande wao wameiomba mahakama kusubirisha rufaa yao ili wasikilize kwanza rufaa ya upande wa jamhuri kwani rufaa zote zimegongana na zinaelekea sehemu moja  



"Unajua leo rufaa mbili zimegongana ile ya upande wa jamhuri na ile ya kwetu sisi,hivyo basi sisis tumeiomba mahakama kusitisha rufaa yetu kusikilizwa kwanza ili ya serikali isikilizwe kwanza,kwani rufaa zote zinaelekea upande mmoja ,wandege apande ndege na wa basi apande basi "alisema Kibatala.


Hata hivyo mbunge huyo wa Arusha mjini Godbless lema amerudishwa rumande hadi hapo maamuzi yatakapotolewa na mahakama.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages