-Ni kinywaji pekee chenye ubora na kinachorahishisha maisha
Kampuni ya TBL Group imezindua Chibuku Super kwenye chupa ya bia ya glasi yenye ujazo wa ML500, chupa hii ni nzuri na ya kuvutia ya glasi inayorudishwa (Returnable) ina ujazo wa nusu lita na itauzwa kwa bei ya shilingi 700/- tu, kwa chupa.
Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi huo uliofanyika katika ukumbi wa kiwanda kilichopo eneo la Pasiansi Mwanza , Meneja Masoko wa TBL Group, Bw. Oscar Shelukindo; alisema “leo ni siku ya furaha kubwa sana kwetu TBL na kwa watumiaji wote wa Bia yetu hi ya asili , kwani tumeweza kuzindua Bia hii ya “Chibuku Super” kwenye chupa ya glasi ambayo inatarajiwa kuleta mapinduzi makubwa katika soko la Bia hapa nchini. Bia hii imetengenezwa kwa utaalamu wa hali ya juu na kwa kutumia mitambo ya kisasa kabisa, hivyo kuwahakikishia wanywaji Ubora wa hali ya juu”
Shelukindo alisema, Bia hii inatengenezwa kwa kutumia malighafi za hapa nyumbani, ikiwemo nafaka ya mahindi na mtama bora toka kwenye ardhi yetu, haya yote yanatupa kila sababu sisi watanzania kujivunia kilicho chetu na kukumbuka asili yetu, kwani hii ni Bia yetu ya asili. Chibuku Super ina kilevi cha asilimia 4, kinachokufanya uweze kuitumia kwa muda mrefu ukiwa na marafiki, lakini pia inakupa lishe nzuri kutokana na virutubisho vinavyopatikana katika nafaka zinazotumika kutengeneza bia hii.
Akizungumzia juu ya usambazaji wa Bia hii, meneja mauzo wa TBL Bw. Fred Kazindogo amesema; Baada ya uzinduzi huu unaofanyika leo, Bia hii ya Chibuku Super kwenye chupa ya ML 500 NA KWA BEI YA 700/-TU itaanza kupatikana kesho kwa wasambazaji wakubwa na katika baa mbliimbali na sehemu nyinginezo zinazouza vileo. “Tunatarajia wateja na wapenzi wa bia wataifurahia bia hii mpya itakayouzwa kwa bei ya shilingi 700/- tu kwa chupa. Kreti itauzwa kwa 14,000/- kwa wasambazaji”
Alisema kwa sasa Bia hii itaanza kupatikana katika mikoa 15 ikiwemo Mwanza, Kagera, Mara, Shinyanga, Geita, Tabora, Singida, Kigoma, Simiyu, manyara , Kilimanjaro, Arusha, Katavi, Mbeya na Rukwa.
Na kwa wauzaji wa jumla, tunatarajia watahamasika kuuza bia ya Chibuku Super kwani ina faida nzuri na bia hii inadumu kwa miezi 4 kwenye soko ambao ni mrefu sana kulinganisha na products zetu nyingine, alisema Kazindogo
“Tuna imani kubwa wapenzi wa Bia wataipokea Chupa hii mpya kwa kwa bei ya 700/- kwa Shangwe na furaha kubwa, na pia watatumia Bia hii kuonyesha kuwa wanajali Asili yao”. Alisema Kazindogo.
Meneja Masoko wa TBL Group, Oscar Shelukindo akionyesha chupa mpya ya chibuku Super katika mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla ya uzinduzi wa chupa mpya
Maofisa Waandamizi wa Masoko na Mauzo wa TBL Group wakionyesha kinywaji cha Chibuku Super katika chupa mpya wakati wa hafla ya uzinduzi jijini Mwanza
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)