Mratibu wa Masoko na Mawasiliano wa Kampuni ya mikopo ya Bayport Financial Services, Mercy Mgongolwa (kushoto), akimkabidhi Ofisa Utumishi wa Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha, Emelda Kisosi, kompyuta kwa ajili ya kusaidia ufanisi wa kazi ofisi zao kama sehemu ya kujitolea kwa jamii. Kulia ni Ofisa TEHAMA wa Halmashauri ya Wilaya Arumeru, Edna Mwaipiana.
Na Mwandishi Wetu, Arusha
HALMASHAURI ya Wilaya Arumeru, mkoani Arusha, jana imepokea kompyuta mbili zilizotolewa msaada na Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services, kama sehemu ya
ushirikiano na kusaidia na kukuza ufanisi wa kikazi kwa watumishi wa umma wilayani humo.
Kompyuta hizo zinatoka ikiwa ni siku chache baada ya Mkoa wa Morogoro nao kupokea msaada
kama huo kwa ajili ya kuboresha utendaji kazi wa watumishi wa umma.
Mratibu wa Masoko na Mawasiliano wa Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services inayojihusisha na mikopo, Mercy Mgongolwa katikati akizungumza jambo katika makabidhiano hayo yaliyofanyika leo jijini Arusha. Kulia ni Ofisa Utumishi wa Halmashauri ya Wilaya Arumeru, Emelda Kisosi.
Akizungumza katika makabidhiano hayo leo jijini Arusha, Mratibu wa Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Mercy Mgongolwa, alisema wamefikisha kompyuta mbili katika wilaya hiyo kama orodha ya mahitaji waliyopokea kutoka Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Alisema anaamini kwa kufikisha kompyuta hizo, kutachangia ufanisi wa kikazi kwa kutumia vyema teknolojia ya kompyuta iliyokuja kupanua wigo wa utendaji bora wa kazi kwa Tanzania nzima kwa hali ya kupanga, kutatibu na kuhifadhi kumbukumbu muhimu za kiutendaji wakati wote.
Picha ya pamoja baada ya makabidhiano ya kompyuta hizo.
Mercy Mgongolwa akikabidhi nyaraka za kompyuta hizo. “Huu ni mwendelezo mzuri wa ugawaji wa kompyuta 205 tulizonunua zenye thamani ya Sh Milioni 500, ambapo tayari kompyuta 125 zimefikishwa Makao Makuu ya Utumishi na wao kutuelekeza eneo na idadi ya ugawaji kwenye halmashauri za nchi yetu,” alisema
Naye Afisa Utumishi wa Halmashauri ya Wilaya Arumeru, Imelda Kisosi, aliwashukuru Bayport kwa kujitolea vifaa hivyo muhimu vitakavyowapatia urahisi watendaji hao kuchapa kazi kwa nguvu zote ili wilaya yao isonge mbele.
“Msaada huu ni mkubwa mno kwetu hivyo tunawashukuru na kuwaahidi ushirikiano wa hali ya juu sanjari na kuwataka Bayport waendelee kuwa karibu na jamii yetu kama njia ya kuwapatia maendeleo Watanzania wote, hususan wa wilayani kwao Arumeru, mkoani Arusha,” alisema Kisosi.
Bayport Financial Services ni taasisi ya mikopo inayojitolea kwa hali na mali ambapo mbali na kununua kompyuta hizo 205, pia imekuwa ikishiriki kujenga madarasa katika shule mbalimbali, hali inayochangia kwa kiasi kikubwa kupanua kiwango cha elimu nchini.
Huduma znazotolewa na Bayport ni pamoja na mikopo ya fedha taslimu kwa watumishi wa umma na wafanyakazi wa kampuni binafsi, mikopo ya viwanja, mikopo ya fedha kwa njia ya simu za mikononi maarufu kama ‘Nipe Boost’, Bima ya Elimu kwa Uwapendao na nyinginezo zinazopatikana katika ofisi zao za matawi 82 katika mikoa na wilaya mbalimbali za Tanzania Bara.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)