Wanafunzi wapatiwa mafunzo ya usalama barabarani - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Wanafunzi wapatiwa mafunzo ya usalama barabarani

 Afisa wa jeshi la polisi kitengo cha Usalama  ,Haji Nduya akitoa mafunzo ya usalama barabarani kwa wanafunzi wa shule ya msingi Oysterbay jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama kanda maalum ya Dar es Salaam chini ya udhamini wa TBL Group,    ikiwa mkakati wa n kupunguza ajali za barabarani.
 Afisa masuala endelevu wa TBL Group Irene Mutiganzi (kulia) akifafanua jambo kuhusiana na  usalama barabarani kwa wanafunzi wa  shule ya msingi ya Oysterbay jijini  ya Dar es salaam   wakati wa   mafunzo ya usalama barabarani kwa wanafunzi  wa shule hiyo.
 Mkaguzi msaidizi wa Jeshi la polisi kitengo cha Usalama barabarani kutoka makao makuu ya Jeshi hilo ,Erick ndidi (kulia) na Afisa  wa Masuala Endelevu wa TBL Group  Irene Mutiganzi (kushoto)wakitoa mafunzo ya usalama barabarani kwa wanafunzi  wa shule ya masingi ya Oysterbay jijini Dar es Salaam
 Mkaguzi msaidizi wa Jeshi la polisi kitengo cha Usalama barabarani kutoka makao makuu ya Jeshi hilo ,Erick ndidi akiowaongoza wanafunzi  wa shule ya masingi ya Oysterbay jijini Dar es Salaam, kuvuka barabara ya Haile Selassie, kwa kutumia alama za barabarani (zebra).
 Mkaguzi msaidizi wa Jeshi la polisi kitengo cha Usalama barabarani kutoka makao makuu ya Jeshi hilo ,Erick ndidi akiowaongoza wanafunzi  wa shule ya masingi ya Oysterbay jijini Dar es Salaam, kuvuka barabara ya Haile Selassie, kwa kutumia alama za barabarani (zebra).
Afisa Mawasiliano wa TBL Group, Amanda Walter akimkabidhi zawadi ya mkebe wenye vifaa vya shule mwanafunzi wa darasa la kwanza katika shule ya msingi Oysterbay jijini Dar es Salaam, Jesca Reginald  mara baada ya kujibu maswali yaliyohusu usalama wa barabarani, wakati wa maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama Kanda maalum ya Dar es Salaam,yaliyodhaminiwa na TBL Group ikiwa ni sehemu ya kupunguza ajali kwa watoto wa shule wakati wanapovuka barabara wakienda au kutoka shuleni.Kushoto ni Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la polisi kitengo cha Usalama barabarani kutoka makao makuu ya Jeshi hilo ,Erick ndidi. 
-Yamedhaminiwa na TBL
 
Katika maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani mkoani Dar es Salaam,mwishoni mwa wiki Jeshi la Polisi Kanda ya mkoa wa Kinondoni liliendesha mafunzo ya usalama barabarani katika shule ya msingi Oysterbay chini ya udhamini wa kampuni ya TBL Group.
 
Wakati wa mafunzo hayo yaliyoendeshwa na askari kutoka Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama barabarani wanafunzi waliweza kufundishwa  alama mbalimbali za bararani,mambo ya kuzingatia wanapokuwa barabarani na jinsi ya kuvuka barabara kwa tahadhari.
 
Pia wanafunzi walipata fursa ya kuuliza maswali mbalimbali kuhusiana na masuala ya  usalama barabarani  na waliulizwa maswali ya  chemsha bongo kuhusiana na  elimu ya mafunzo  waliyopatiwa.
 
Afisa mawasiliano wa TBL Group,Amanda Walter, alisema kuwa  TBL imedhamini mafunzo haya ikiwa ni mwendelezo wake wa kuunga mkono jitihada za serikali  za kushirikiana na Jeshi la Polisi  katika kampeni za usalama barabarani.
 
“Kampuni ya TBL  tunao mkakati wa kuendelea kushirikiana na serikali kupitia kikosi cha Polisi wa Usalama barabarani na wadau wengine kuhakikisha tunapunguza matukio ya ajali za barabarani nchini ambazo zimekuwa zikisababisha vifo,ulemavu na hasara kwenye jamii”.Alisema.
 
Alisema mpango wa kuwafikishia wanafunzi wa shule za msingi elimu ya usalama barabarani hauna budi kuungwa mkono kwa nguvu zote  kwa kuwa wakielewa tatizo hili mapema itakuwa ni rahisi kutokomeza tatizo hili katika siku za usoni. “Wanafunzi wana uelewa mkubwa na ni rahisi kushika wanayofundishwa pia wanaishi katika mazingira ambayo ni muhimu kuwa na ufahamu wa masuala haya”.
 
Mbali na kudhamini mafunzo haya ya wanafunzi kampuni ya TBL Group imekuwa mmoja wa wadhamini wakuu wa Wiki ya Nenda Kwa Usalama ngazi ya kitaifa ambapo ilitoa vifaa mbalimbali vya uhamasishaji ikiwemo gari maalumu ya kupimwa afya za madereva la Zahanati inayotembea maarufu kama ‘Zahanati Mwendo’,huduma ambayo ni ya kwanza nay a aina yake nchini ambayo  mpaka sasa inaendelea kuchangamkiwa na madereva popote linapopita gari hilo.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages