Katika jitihada za kutokomeza ajali za barabarani nchini,kampuni ya TBL Group imetoa mchango wa shilingi milioni 11/- kwa ajili ya uhamasishaji wa usalama katika wiki ya Nenda kwa Usalama mkoani Ruvuma.
Akiongea wakati wa hafla ya kukabidhi mchango huu iliyofanyika katika ofisi za Makao Makuu ya Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani mjini Songea ,Meneja Mauzo kutoka TBL Group,Abubakari Masoli,alisema kuwa msaada huu ni mwendelezo wa kampuni kushiriki katika kampeni za Usalama barabarani.
“TBL Group ikiwa ni kampuni inayotengeneza vinywaji vyenye kilevi kwa muda mrefu tumekuwa tukifanya kazi na serikali kupitia Jeshi la polisi katika kampeni za kuhamasisha usalama barabarani lengo kubwa likiwa ni kutokomeza matukio ya ajali nchini kupitia kampeni yetu ya usalama na Unywaji wa Kistaarabu”.Alisema.
Alisema mbali na msaada huo mwaka huu imekuwa mmoja wa wadau waliofanikisha Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani ngazi ya kitaifa iliyofanyika kitaifa mkoani Geita ambapo pia iliweza kuzindua huduma ya gari maalumu la kupima afya za madereva ambalo linajulikana kama ‘Zahanati Mwendo’ambalo limewezesha madereva wengi kupima afya zao na kupatiwa matibabu.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Songea, Pololet Mgema,kwa niaba ya serikali aliishukuru TBL Group na wadau wengine ambao wanashirikiana na Jeshi la Polisi kufanikisha kampeni za usalama barabarani.
Alisema bado kuna matukio mengi ya ajali nchini ambazo zinasababisha vifo vya watu wengi na kuleta hasara nyingi hivyo kunatakiwa jitihada za pamoja kufanya kampeni ya kuzipunguza ikiwezekana hata kuzimaliza kabisa.
Mwakilishi wa TBL Group ,Abubakari Masoli ambaye ni Meneja Mauzo wa kampuni hiyo akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi mchango wa kampuni kwa ajili ya kufanikisha Wiki ya Nenda kwa Usalama mkoani Ruvuma
Mkuu wa wilaya ya Songea Pololet Mgema (kulia )akipokea mfano wa hundi ya Tsh,Milioni kumi na moja kutoka kwa Mwakilishi wa TBL Group,Abubakar Masoli (kushoto) kwa ajili ya kufanikisha maadhimisho ya Nenda kwa Usalama barabarani,wengine pichani ni Maofisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi mkoani humo.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)