-Kaya 65,000 tayari zimeunganishwa kanda ya Afrika Mashariki
Kampuni ya kimataifa ya kusambaza umeme wa jua na vifaa vinavyotumia nishati hiyo kutoka Ujerumani ya Mobisol Tanzania katika jitihada zake kuhakikisha ineleta mabadiliko kwenye jamii kupitia kuiwezesha kupata umeme wa uhakika na wa gharama nafuu imetoa msaada wa kufunga umeme wenye Wp 200 kwa shule ya msingi Majengo iliyopo wilayani Bagamoyo.
Hafla ya kukabidhi msaada huo imefanyika katika shule ya msingi ya Majengo ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Dorris Mwakatebe na ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka sekta ya elimu wilayani humo na wakazi wa Bagamoyo.
Msaada huo ni mkakati wa kampuni ya Mobisol kusaidia huduma za jamii kwenye maeneo inayofanyia shughuli zake na kuendeleza jamii kupitia kuzipatia nishati ya umeme na kuwezesha wanafunzi kusoma katika mazingira bora.
Umeme huo utanufaisha zaidi ya wanafunzi 1,000 na walimu 44 ambapo utawawezesha kuwasha taa na matumizi ya vifaa mbalimbali na utawezesha wanafunzi kujisomea katika mazingira bora nyakati na usiku ikiwemo walimu kufanya vizuri maandalizi ya masomo.
Bi.Dorris Mwakatebe kutoka ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo,ameishukuru kampuni ya Mobisol kwa msaada huo ambao umelenga kukuza sekta ya elimu kwa kuwawezesha wanafunzi kusoma katika mazingira bora ikiwemo walimu kufanya kazi katika mazingira bora.
“Umeme huu utawezesha walimu kusikiliza redio,kuangalia vipindi vya kielimu kipitia luninga ,kuchaji simu zao na matumizi ya kompyuta kwa ajili ya kuperuzi interneti kwa ajili ya kupata taarifa mbalimbali zikiwemo za maarifa ya kielimu,tuna imani kubwa utaleta mabadiliko makubwa na kiwango cha ufaulu kuongezeka”.Alisema.
Mwalimu Mkuu wa shule ya Majengo Lukama Lukama, alishukuru msaada huu na alisema utawezesha wanafunzi kusoma katika mazingira bora na kujifunza masomo mbalimbali kwa vitendo tofauti na hapo awali ambapo shule ilikuwa haijafungiwa umeme pia utawezesha walimu kufanya maandalizi ya masomo kwenye mazingira bora.
Meneja Masoko wa Mobisol Seth Mathemu alisema “Tunafurahi kutoa msaada huu wenye kuleta mabadiliko kwenye jamii na huu ni moja ya mkakati wa kampuni kutumia sehemu ya faida yake kusaidia huduma za kijamii hususani katika sekta ya elimu ,afya na utunzaji wa mazingira”.
Alitoa wito kwa familia kwenye maeneo ambayo hayajafikiwa na umeme wa gridi ya taifa kujiunga na umeme wa uhakika na gharama nafuu wa Mobisol ili waweze kufurahia na familia zao hususani msimu wa sikukuu ya Krismas na mwaka mpya “Ni wakati wa watanzania wasiofikiwa na nishati ya umeme kujiunga na Mobisol ili waondokane na matumizi ya mafuta ya taa na kuweza kutumia vifaa vya maisha ya kisasa ikiwemo kujiongeza kiuchumi kupitia nishati ya umeme”.
Hadi kufikia sasa umeme wa teknolojia ya kisasa wa Mobisol umeweza kufikia kaya na taasisi mbalimbali zaidi ya 65,000 katika ukanda wan chi za Afrika Mashariki.Ili kuhakikisha umeme unawafikia wananchi wengi kwa urahisi na kwa unafuu imeanzisha mpango wa kuwaunganisha wananchi nishati ya umeme inayowawezesha kulipa gharama za kuunganishwa kwa awamu mpaka kwa kipindi cha miaka mitatu ambapo wanaweza kufanya malipo hayo kptia simu zao za mkononi.
Wanafunzi wakipatiwa maelezo ya kutunza vifaavya umeme ambavyo vimetolewa na Mobisol Tanzania
Wanafunzi wakishangilia kupata nishati ya umeme
wanafunzi wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Mobisol katika hafla hiyo
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)